Majadiliano
kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi
kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini
yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31
jijini Dar es Salaam.
Taarifa
ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema
kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa
Palamagamba Kabudi.
Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.
Profesa
Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri
kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya
madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya
nchi ipasavyo.
Williams imeelezwa ameshukuru uwepo wa majadiliano
hayo, akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na
ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande
zote mbili.
Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za
kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na
nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi
kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.
Monday, July 31, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Nimebahatika kupata fursa kadhaa kukaa na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa enzi za uhai wake....
-
Na Mathias Canal, WAZOHURU MEDIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali...
-
Na THEOFLIDA WA YESU Naanza kwa kuwasalimu kwa JINA LA YESU. Jina lililo Kuu kupita majina yote. Wiki ...
-
Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto ...
-
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Mgombea nafasi ya Udi...
Powered by Blogger.





0 comments:
Post a Comment