Monday, July 31, 2017

Majadiliano kati ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold yaanza

Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya nchi ipasavyo.

Williams imeelezwa ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo, akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.

Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment