Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar
Jangombe Boys asubuhi ya leo imeondoka Unguja na kuelekea kisiwani Pemba kwa lengo la kuchukuwa point sita kwenye mechi mbili.
Timu imefika salama na imepokelewa kizalendo na wapezi wa Boys Pamoja na viongozi wa Friends of Boys waliotangulia wiki kabla kwa lengo la kwenda kuandaa mazingira mazuri ya makazi kula na eneo la kufanyia mazoezi muda wote wa siku nane ambao timu inakuwa Pemba alisema Alawi H. Foum Katibu wa Friends of Boys.
Alawi aliongeza kwa kusema viongozi waliotanguliwa wamefanikisha maandalizi yote na timu itaishi Pemba bila ya usumbufu timu iko Piki tunafarajika kupata mapokezi ya nguvu kutoka bandarini hadi tunaingia Piki imani yetu malengo yetu ya Kurudi na point sita yatatimia na jioni ya leo timu imefanya mazoezi mepesi katika kiwanja cha Jambieni kujiaandaa na mchezo wa awali zidi ya Mwenge na ule wa pili zidi ya Okapi
Alawi alipoulizwa juu ya wachezaji waliosafiri kama wapo fiti alisema wachezaji wako sawa hasa waliosafiri ukiachilia mbali wachezaji watatu ambao wamesafiri na combain ya wilaya ya mjini iliyokwenda Arusha kushiriki mashindano ya Rolling stone na Abdi kassim Babi atawasili Pemba kesho baada ya kuweka sawa mambo yake ya familia
Friends Of Boys imejipanga na ahadi zake zipo pale pale tuwaombe wapezi na wadau wote wa Boys waiombee timu irudi na point sita kwa kushinda mechi zote zidi ya Mwenge na Okapi ili timu ijiweke sehemu nzuri ya kufikia malengo yake ya kuchukuwa ubingwa.
0 comments:
Post a Comment