Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu.
Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo – hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa.
Mchango wa mabadiliko ya mazingira
katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote.
Idadi kubwa ya
‘wakimbizi wa mazingira’ sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa
ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii
inategemewa kundelea kuongezeka.
Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa
Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka
2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao
kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama
kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na
Ulaya.
Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu
zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa
jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea
ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya
kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa
elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa.
Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili:
Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa
usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda
kiwango chake cha uzalishaji. Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas
Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa
ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya
matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi
hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia
huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali.
Hii ndio
sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika
kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame,
kuenea kwa jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na
usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa
unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI).
Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu
wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia
mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa
jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi
husababisha watu kuyahama makazi yao.
Katika kutafuta na kuendeleza
elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa
wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, Programu
ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga
fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali
zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu
katika makazi yao.
Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa
hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia
kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali
endelevu na imara kwa wote.
Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova,
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na
Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017
0 comments:
Post a Comment