METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, June 18, 2017

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO AONGOZA TIMU YA WAKUU WA IDARA KATIKA UKAGUZI WA MAANDALIZI YA MAONYESHO YA NANENANE KIJIJI CHA ITUNGI MOROGORO


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndg John Lipesi Kayombo leo ameambatana na timu ya wakuu wa idara wa Manispaa ya Ubungo kutembelea na kijionea maandalizi ya Nanenane katika eneo la Itungi Mkoani Morogoro.

Akiwa katika eneo hilo la  Manispaa ya Ubungo maalum kwa maonesho ya Nanenane mkurugenzi na timu yake wamejionea aina mbalimbali za mazao ambayo tayari yamepandwa kama ,.Nyanya, Bilinganya nene na ndefu, nyanya chungu,mchicha nafaka, mbaazi pilipili hoho, mbuzi, na pilipili ndefu, mwidu, kabichi nyeupe,kabichi nyekundu, karoti, beetroot, mint viungo, mahindi , mihogo, viazi vitamu,passion, mipapai, michugwa, miembe na migomba.

Pia Manispaa tayari imetengeneza bwawa la kisasa la samaki aina ya Tilapia, na banda la kisasa la ng'ombe ,

Baada ya kuona maandalizi hayo mkurugenzi amewapongeza idara ya kilimo kwa maandalizi hayo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuwezesha pale patakapohitaji uwezeshwaji yuko tayari ili kuhakikisha maonyesho hayo yanakuwa ya tofauti licha ya Ubungo kuwa ni Halmashauri mpya .

Naye kaimu mkuu wa idara ya kilimo na mifigo ndg Salimu Msuya amesema wao kama idara wamejipanga vizuri wanaamini watafanya vizuri katika maonyesho hayo wanawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la Ubungo siku hiyo ya Nanenane.

Tarehe 8/8/ kila mwaka Tanzania huadhimisha sikukuu ya wakulima.

Ubungo mpya, Ubungo ya tofauti 
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com