METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 24, 2017

Ujenzi barabara Bigwa – Kisaki mbioni kuanza

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani

Na Magnus Mahenge, Dodoma

SERIKALI inatekeleza mradi wa ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Bigwa- Kisaki kwa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena, aliyetaka kujua ni lini ujenzi wa barabara ya Bigwa Kisaki yenye urefu wa kilometa 78, utaanza ili wananchi waliowekewa alama ya kubomolewa nyumba waanze maandalizi maeneo ya kuhamia.

Ngonyani alisema utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na usanifu wa madaraja ya Ruvu-Mvuha kwa gharama ya Sh milioni 713.5. Alisema Usanifu huo utakamilika mwishoni mwa Juni mwaka huu, ambapo usanifu wa Daraja la Duthumi umeshakimilika.

Alisema upembuzi ukikamilika, serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami pamoja na madaraja. “Serikali inaendelea kuifanyia matengenezo barabara hiyo ili kuendelea kupitika wakati wote wa mwaka. “Katika mwaka wa fedha 2016/17, zimetengwa Sh milioni 807.84 na mwaka wa fedha 2017/18, zimetengwa sh bilioni 1.12,” alisema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com