SERIKALI itaendelea kuwawekea mazingira bora watoto kukua kiafya,
kielimu na kimaadili na kuwaondolea vikwazo katika maendeleo ikiwemo
kuhakikisha kuwa idadi ya watoto 35,916 wanaoishi na kufanya kazi
mitaani wanapungua kwa asilimia 50.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Hamisi Kigwangalla alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Alisema Tanzania kuna watoto wanaokadiriwa
kufikia asilimia 50.1 ya jamii nzima na watoto hao wanahitaji kupatiwa
haki za msingi ikiwemo elimu, afya, ulinzi na malezi bora bila ubaguzi.
Dk Kigwangalla alisema serikali imekuwa ikiweka mazingira bora ya
watoto ili waweze kukua kiafya, kielimu na kimaadili kwa kuwaondolea
vikwazo katika maendeleo yao. Alisema mpango wa taifa wa kutokomeza
ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utatekelezwa katika kipindi
cha miaka mitano unatarajia kumaliza tatizo la ukatili kwa watoto kwa
asilimia 50 ifikapo mwaka 20121/2022.
Alisema malengo hayo yatafikiwa kwa kuhakikisha kuwa idadi ya watoto
35,916 wanaoishi na kufanya kazi mitaani wanapungua kwa asilimia 50. Pia
kupunguza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka
asilimia 29 hadi asilimia tisa, kuimarisha huduma ya elimu kwa watoto wa
kike wanaotoka katika familia maskini kutoka asilimia 23.4 hadi
asilimia 53.4 Alitaja juhudi nyingine ambazo serikali imefanya katika
kuendeleza haki na ustawi wa watoto hapa nchini ni pamoja na kutoa elimu
ya malezi na makuzi ya mtoto katika ngazi ya familia, shule katika
halmashauri 74 ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto wa kike.
Pia kuanzishwa kwa timu ya ulinzi wa mtoto katika halmashauri za
wilaya 63 ili kuboresha utoaji huduma stahiki kwa watoto walioathiriwa
na vitendo vya ukatili. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la watoto
wa Tanzania, Joel Festo, aliwataka watoto kusoma kwa bidii kwani wakati
Tanzania inatekeleza sera ya uchumi wa viwanda itahitaji wataalam wengi.
CREDIT: HABARI LEO
Monday, June 19, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment