HIFADHI ya Pori la Akiba la Selous imepata ufadhili wa Sh bilioni
47.124 kutoka Ujerumani kwa ajili ya mradi wa miaka mitano wa Maendeleo
ya Uhifadhi wa Ikolojia ya Pori la hifadhi hiyo (SECAD).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa
kushirikiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke
alizindua mradi huo ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa
ushirikiano na Serikali ya Tanzania, mradi huo utatekelezwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania, WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological
Society).
Akizungumza katika hafla iliyofanyika jana, Matembwe Selous Mkoani
Morogoro, Maghembe alisema Serikali ya Ujerumani kupitia benki ya KFW
ilichangia Euro milioni 18 (sawa na Sh bilioni 45.124) katika mradi huo
wa miaka mitano huku mashirika ya WWF (World Wildlife Fund) na FZS
(Frankfurt Zoological Society) kwa pamoja zikachangia Euro 400,000 (sawa
na Sh bilioni 2).
Profesa Maghembe alisema, “Mradi huu ni muhimu kwa kuwa utasaidia
kuongeza nguvu kwenye jitihada zetu za kuendeleza na kuimarisha hifadhi
ya pori hili la Selous ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi pamoja na
kutuongezea nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili.”
Alisema jitihada ambazo Serikali imeshazifanya katika pori hilo ni
pamoja na kuimarisha doria za ndege zenye rubani na zisizo na rubani
(drones), kutoa mafunzo ya jeshi usu kwa askari, kuongeza maaskari
pamoja na vitendea kazi ambapo katika mwaka ujao wa fedha Serikali pia
itatoa magari mengine 15 kusaidia pori hilo.
“Pamoja na jitihada hizo tuna mpango wa kuwekeza dola za Marekani
milioni 156 (sawa na Sh bilioni 352.560) kwa ajili ya kuboresha pori
hili (Selous), Ruaha, Mikumi, Ruangwa na Kitulo kuhakikisha watalii
wanatembelea maeneo haya na kuondoa kile kikwazo cha wao kutotembelea
hifadhi za Kusini, hiyo inaenda sambamba na kuimarishwa kwa shirika la
ndege la Serikali la Air Tanzania kuondoa changamoto iliyokuwepo ya
usafiri wa anga”, alisema.
Akizungumzia changamoto ya ujangili katika pori hilo, alisema
Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hilo ambapo
majangili wengi wameshakamatwa katika maeneo ya Tunduru, Namtumbo na
maeneo ya katikati ya Selous.
Alisema changamoto hiyo, bado ipo katika maeneo ya Mkoa wa Ruvuma,
ambapo imeripotiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kuwa kuna
upatikanaji mkubwa wa silaha za kivita kutoka nchini Msumbiji, ambazo
zinapatikana kwa watu kubadilishana na magunia ya mchele, changamoto
ambayo inaendelea kufanyiwa kazi.
CREDIT: HABARI LEO
Monday, June 19, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment