Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amekutana na Viongozi wa Ubalozi wa China Leo katika Ofisi Ndogo Lumumba kujadili Mambo Mbali Mbali ya Kiutendaji kichama na Kiserikali na Ugeni huo umeongozwa na;
Cde:Dong Zhenyu, Katibu wa Balozi wa China Nchini Tanzania,
Cde; Dai Xu Counsellor wa China Nchini Tanzania Pamoja na Ndg George Daniel Afisa Idara ya Siasa na Uhusiano KimaTaifa na baadhi ya Watendaji Idara ya Itikadi na Uenezi.
Lengo la ugeni huo lilikuwa ni kujifunza Uzoefu wa Chama Cha Mapinduzi Jinsi kinavyoendesha Mafunzo Kwa Makada, Nafasi ya Chama Tawala Nchini Tanzania,Utendaji wa Chama,Uteuzi wa Makada ktk kukitumikia Chama na Serikali.Lakini pia Uendeshaji wa Mafunzo kichama
Ndg Humphrey Polepole aliwafafanulia na kuelezea jinsi Chama kilivyokuwa kikitoa Mafunzo Mbali Mbali kuanzia 1961 hadi 1991 wakati wa Chama Kimoja yaani TANU baadaye CCM hadi sasa.
Ndg Humphrey Polepole alitaja Baadhi ya Vyuo vya Mafunzo hayo vilikuwa kama ifuatavyo;
Kivukoni College Kigamboni- Dar Es Salaam, Lushoto -Tanga, Ilonga Kilosa, Hombolo- Dodoma, Msaginya- Rukwa, Murutunguru- Ukerewe.Vyote hivyo Vilikuwa ni Vyuo vya Mafunzo ya Uongozi kwa Makada na Watendaji wa Serikali Kuanzia Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Kabla na baada ya Uteuzi.
Counsellor wa Balozi wa China Nchini Tanzania ndg Dai Xu amepongeza Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa jinsi kilivyo na Mfunzo Mzuri kwa Kuwaandaa Makada na Viongozi ktk kulitumikia Taifa la Tanzania.
Uongozi wa China Nchini Tanzania kwa niaba ya Serikali ya China na Chama Tawala CPC umeahidi kushirikiana na CCM ktk Kuimarisha Mafunzo kwa Vijana na Makada wa Chama Tawala ili kuendeleza Umoja na Mshikamano ulioasisiwa na Waasisi wa Mataifa yote Mawili yaani Tanzania na China.
0 comments:
Post a Comment