Waziri
wa nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI )
Mhe. Selemani Jafo, amewaagiza wakala wa Majengo TBA Mkoani Iringa, kurudia
ukarabati wa sakafu za madarasa ya Sekondari kongwe ya Malangali baada ya
kubaini kuwa imejengwa chini ya kiwango, huku akipongeza ujenzi wa kituo cha
Afya Malangali unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa mtindo wa
‘Force Account’
Waziri Jafo, ametoa
agizo hizo wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya
Malangali, baada ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa shilingi milioni
400 za kutekeleza mradi huo.
Jafo, amesema yeye
kama Waziri mwenye dhamana na Shule hapa nchini, hawezi kuvumilia anapoona
Taasisi ya Serikali inatekeleza mradi chini ya ya kiwango wakati inalipwa
mabilioni ya fedha za umma.
“Halafu mimi Jafo Shule zipo chini yangu
unafikiri nitakubali “I never” ni bora mngeacha Sakafu ya kwanza, Taasisi ya
Serikali ni lazima ifanye kazi ya Serikali kiusahihi na si kiujanja
ujanja kama hivi, nenda mkaone Majengo ya Kituo cha Afya hapo jirani
yaliyojengwa kwa Force account, Majengo ni mazuri yanaubora chini yamewekwa
“tiles” alisema Waziri huku akigonga viatu vyake kwenye sakafu
ambayo ilionesha vyufa kadri alivyokuwa akigonga.
Akijibu hoja za Waziri,
fundi Mkuu wa TBA katika mradi huo Bi.Agnes Haule, amekili udhaifu
wa ujenzi na kufafanua kuwa, sababu ya tatizo hilo linatokana na uamuzi wa
kusakafia kabla ya kukauka kwa zege kutokana na uhitaji wa vyumba vya kusomea
na kuongeza kuwa wapo tayari kurudia kazi hiyo.
Awali akikagua
maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Malangali, unaotekelezwa kwa mfumo wa
force account kwa kutumia mafundi wenyeji Mh. Jafo, amefarijika na maendeleo ya
ujenzi huo kwa kuwa umezingatia viwango na thamani ya fedha.
“Kazi hii inamaanisha kwamba tunauongozi
mzuri wa Halmashauri ya Mufindi na Wilaya nzima ya Mufindi na
hakikisheni mnamaliza kazi hii ikiwa salama, nimeangalia vitu mbalimbli, kuta
zenu na ujenzi kwa ujumla mko vizuri. Aidha, mnavyofanya vizuri mnatushawishi
zaidi kwamba siku nyingine tunapokuwa na mradi, tuifikirie Mufindi kwanza na
haya ndiyo mambo ambayo Mheshimiwa Rais anataka kuyaona
na si vinginevyo”
Mnamo mwezi wa 12/ 2017, Halmashauri ya Mufindi ilipokea kiasi cha
shilingi milioni 400 kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ili zitumike kufanya utanuzi
wa kituo cha Afya Malangali unaojumuisha, Nyumba ya Mganga, Maabara, Chumba cha
upasuaji na Wodi ya Mama na Mtoto na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi 01/2018 na
unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa 06.
0 comments:
Post a Comment