METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 8, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AFANYA ZIARA YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amefanya ziara ya kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Jimbo lake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Minazi Mitatu kata ya Kitangiri uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt Leonard Masale na Mkurugenzi wa Ilemela John Wanga

Akizungumza katika mkutano huo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kushukuru viongozi wenzake wa wilaya ya Ilemela kwa namna wanavoshiriki kwa pamoja katika kutatua kero za wananchi amewataka wananchi wa Ilemela kutimiza wajibu wao kwa kulipa Kodi mbalimbali za Ardhi huku akiwaasa juu ya kutumia fursa ya uwakilishi  wake Bungeni katika kutatua kero zao

‘…Lakini nishukuru sana Timu ya wilaya tunafanya kazi kwa kushirikiana na ndo mana tumekuja wote hapa likitokea la kutokea Mbunge hayupo lakini ujue unamuona nani Halmashauri, Niwaombe vikao vya Bunge vinaendelea mjini Dodoma nitumeni nikawasemee  sambamba na hilo niwaombe ndugu zangu tulipe kodi za Ardhi kama utashindwa kulipa yote kwa pamoja nenda ofisi za Halmashauri kaa nao chini wakupe utaratibu hata wa kulipa kwa awamu kidogo kidogo kuliko kuacha kabisa kwani hasara yake ni kubwa …’ Alisema

Akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt Leonard Masale mbali na kuhimiza vita dhidi ya madawa ya kulevya  amemuhakikishia Mbunge huyo kuendelea kushirikiana katika kuwaletea wananchi wa wilaya yake kutekeleza shughuli za maendeleo

Akihitimisha mkutano huo mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga mbali na kumshukuru kwa namna anavyoshiriki katika utatuzi wa changamoto za wananchi pamoja na majukumu ya kitaifa aliyonayo huku akiwaasa wananchi hao kuwatumia vizuri viongozi wao katika kutatua kero zao

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
08.07.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com