Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Jimbo la Kikwajuni leo wameandaa Mashindano ya kuhifadhi Qur-an kwa kushirikisha vyuo vya ndani ya jimbo lao na mualiko wa vyo vya nje ya Jimbo miongoni mwa vyuo walivyo vialika ni vyuo vya Jimbo la Chumbuni.
Mhe Ussi Salum Pondeza Mbunge wa CCM Jimbo la Chumbuni amehudhuria hafla hiyo kuitikia mualiako aliopewa.
Nimekuja hapa kwa mualiko rasmin tumekuwa na kawaida ya kualikana inapotokea kufanya matukio makubwa mbali mbali binafsi leo nipokea mualiko huu kwa mikono miwili mimi na wananfuzi wote wanaotoka Jimbo langu la Chumbini alisema Mh Pondeza.
Pia hakusita kuelezea wivu uliompata kupitia Mashindano hayo na kuahidi kupitia taasisi yake inashuhulika na elimu Jimboni kwake ya PONDEZA Foundation itafanya Mashindano kama hayo Jimboni kwake mwakani.
Nipo hapa kwa kujifunza kuchukuwa uzoefu nimemwita katibu wangu aje hapa ili tusaidiane kukopi hili adhimu na muhimu tukitoka hapa tukaaze maandalizi ikimpendeza Allah mwakani Jimbo langu tufanye zaidi ya tutakachosoma hapa.
Mh Pondeza aliwaombea dua wanafunzi wote wanaoshiriki Mashindano hayo wafanye vyema Hususan wale wanaotoka Jimbo lake ambao jumla yao wapo watano wameshiriki mashindano hayo kwa Juzuu tofauti alitaja majina ya wanafunzi hao ni.
1. Saada Said Bakar Juuzuu (2)
2. Mustapha Iddi Saleh Juzuu (1)
3. Moh'd Juma Hamad Juzuu (12)
4. Zuhura Shekhe Ali Juzuu (5)
5. Thuwaiba Suleiman Ali.
Mh Pondeza aliongeza kuwa pamoja na kuwa wahusika wameandaa zawadi kwa washindi ila na yeye amewaahidi zawadi nzuri wanafunzi wa Jimbo lake wakifanya vizuri na kuwataka wasiwe na hofu yeye yupo kwa ajili ya kuwaunga mkono.
Mwisho Mh Pondeza aliwashukuru kamati ya maandalizi kwa kazi nzuri waliofanya binafsi sijaona mapungufu na nitachukuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hii ili wakatowe muongozo Jimboni kwangu Pia natoa wito kwa viongozi wezangu wa majimbo ambao bado hawajafikiria kufanya jambo la Kheri kama hili waandae ili wajiwekee akiba kwa Allah maana jambo hili faida yake siku moja utaikuta kwa Allah nawaombea dua waliozaa wazo hili mungu awatie nguvu jambo hili lifanyike kila mwaka INSHAALAH.
0 comments:
Post a Comment