Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa
Arusha Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada
huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania
Picha ikionyesha wa kwanza kulia
Mbunge wa viti maalum (CCM) Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais
John Magufuli msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda 25
katika kituo cha afya cha Levolosi ,ambapo msaada wa vitu hivi
umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja
wapo ya ahadi zakealizozi toa katika kipindi cha kampeni ,katikati ni
Mganga mkuu wakituo cha Afya cha Levolosi Feksi Edward ,wa kwanza
kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha)
Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi wa jiji la Arusha
Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji mara
Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda, mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
Alisema k uwa kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi za Rais na kusema kuwa afanyikitu chochote
Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji mara
baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda, mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
Na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na
kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitiada za maendeleo ambazo
zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada
hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.
Aidha kumekuwa na baadhi ya watu
wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya Rasi kitu ambacho sio
kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea
maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na
mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha
Catherine Magige wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi vitanda 25
,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano
wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi
“Rais wetu anafanyakazi mtu anaesema
afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili
angalieni jinsi alivyozuia makontena ya madini,angalieni jinsi
alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya
kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu
wawananchi wa mkoa wa Arusha na ameamua kutoa msaada wa magodoro
,mashuka pamoja na vitanda “alisema Magige
Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga
mkono kazi ziazofanywa na Rais ,pia alitumia muda huho kuwasihi
madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo
vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa
vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi
Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo
mkurugenzi wa jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali
kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa
hivyo vilivyotolewa huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya
aina mbalimbali.Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda
25 uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa
na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwani moja ya utekelezaji
wa ilani ya chama cha mapinduzi
0 comments:
Post a Comment