Saturday, June 24, 2017


Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha  Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Picha ikionyesha  wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum (CCM) Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais  John Magufuli msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda  25 katika  kituo cha afya cha Levolosi  ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa  na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zakealizozi toa katika kipindi cha kampeni  ,katikati ni Mganga  mkuu wakituo cha Afya cha Levolosi  Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha) Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo Mkuu  wa wilaya ya Arusha  Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi  wa jiji la Arusha
Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji  mara
baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo
Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda, mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
Na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitiada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.
Aidha  kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya   Rasi kitu  ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema
 Hayo yamesemwa   leo jijini hapa  na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha  Catherine Magige  wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi  vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi
Alisema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote
“Rais  wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena  ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na  ameamua kutoa msaada wa  magodoro ,mashuka pamoja na vitanda “alisema Magige
Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi
Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha  Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

No comments:

Post a Comment