METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 17, 2019

MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI WAKATI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIKABIDHIWA UENYEKITI WA SADC LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivalishwa Beji kama ishara ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kutoka kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre JNICC jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Wakuu mbalimbali wa nchi za SADIC wakati wa wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kuaza kwa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC)
Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Wake wa Marais pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akihutubia katika mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob akifurahia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa katika mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Ndani cha Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emerson Mnangagwa kwa ajili ya kikao cha Wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa mara baada ya kuhutubia katika wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi . PICHA NA IKULU
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com