Na Fransisca Emmanue
MKURUGENZI wa Kampuni ya Travel House Global, Sojan Varghese
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na
mashitaka ya kujipatia Dola za Marekani 88,012 (Sh milioni 184.8)
alizopewa kwa ajili ya mahujaji zaidi ya 119 wa Chama cha Karismatiki
Katoliki Tanzania.
Varghese alidaiwa kuchukua fedha hizo kutoka kwa John Ngotty kwa
lengo la kukata tiketi za ndege kwa mahujaji hao waliokuwa wakitaka
kusafiri kuelekea nchi za Roma, Italia na Israeli kwa ajili ya hija.
Akisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard
Mashauri, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai kuwa Desemba 23, 2016
maeneo ya ofisi za Kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Jamhuri, mshitakiwa
alijipatia Dola za Marekani 7,012 kutoka kwa Ngotty fedha ambazo ni kwa
ajili ya nauli ya kupata tiketi ya ndege kwa Wakarismatiki 119 kutoka
Dar es Salaam kwenda Roma nchini Italia na Israel.
Pia alidai, Desemba 23, mwaka jana, maeneo ya ofisi hiyo, mshitakiwa
alijipatia Dola 9,500 kupitia hundi namba 000005 kutoka kwa Ngotty kwa
ajili ya kuwakatia tiketi ya ndege kwenda nchi hizo.
Mkini alidai katika mashitaka ya tatu kuwa, Januari 11, mwaka huu
maeneo ya ofisi hizo, Varghese alijipatia Dola za Marekani 9,500 kutoka
kwa Ngotty kwa lengo la kutumika kununulia tiketi za ndege kwa wanachama
wa Wakarismatiki 119 kwenda hija Roma na Israel.
Katika mashitaka ya nne, mshitakiwa alidaiwa Januari 11, mwaka huu,
alijipatia Dola za Marekani 9,500 kwa hundi namba 000008 kutoka kwa
Ngotty. Aidha, inadaiwa Januari 31, mwaka huu, Varghese alijipatia Dola
za Marekani 37,500 kutoka kwa Ngotty kwa ajili ya nauli ya tiketi ya
ndege kwa wanachama 199 wa Karismatiki.
Mkini alidai, Aprili 12, mwaka huu, maeneo ya Ofisi za kampuni yake,
alijipatia Dola za Marekani 15,000 kutoka kwa Ngotty kwa ajili ya
kununulia tiketi kwa wanachama 119 wa Karismatiki waliokuwa wanakwenda
hija nchi za Roma na Israeli.
Saturday, June 24, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment