METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 16, 2017

WAUZAJI WA CD/DVD ZISIZO NA STIKA WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA MANISPAA YA UBUNGO KUPATIWA UTARATIBU MPYA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawataarifu wafanyabiashara wote wanaouza CD na DVD za Filamu na Muziki zisizo na Stika, Wamiliki wa Maktaba za Kukodisha mikanda ya Video, Wamiliki wa Vibanda vinavyoonyesha picha za Video na wamiliki wote wa Studio za kurekodia Kanda za DVD kuwa wanatakiwa kufika Ofisi za Utamaduni zilizopo Kibamba CCM kwa ajili ya kupatiwa utaratibu mpya wa uendeshaji wa Biashara hii, Ikiwa ni pamoja na Kujisajili.

Zoezi hili litadumu kwa muda wa siku kumi Tu kuanzia Tarehe 19/06/2017 Hadi Tarehe 30/06/2017.

Kwa Yeyote ambaye hatafika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com