Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni, Omary Abdallah na mwenzake,
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kuomba na kupokea rushwa.
Akisoma
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Respicius Mwijage, Mwendesha
Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa(Takukuru), Emanuel
Jacob alimtaja mshtakiwa mwingine kuwa ni George Barongo ambaye ni
mfanyabiashara.
Alidai
kuwa, kati ya January na Februari 12/ 2017, Omary akiwa mwajiriwa wa
Mahakama ya Mwanzo Kinondoni aliomba rushwa ya Sh 205,000 kutoka kwa
Agnes Nyenza kwa ajili ya kumsaidia kwenye kesi yake ya mirathi ya namba
570/2016 ambayo ilikuwa mbele yake.
Alidai,
shtaka la pili linalomkabili hakimu hiyo pia anadaiwa kupokea rushwa
ya kiasi hicho cha fedha Kutoka kwa Nyenza ili aweze kumsaidia katika
kesi hiyo.
Alidai
kati ya Februari na Machi mwaka huu, jijini Dar es salaam, Hakimu Omary
akiwa na mfanyabiashara Barongo waliomba rushwa ya Sh 1,000,000 kutoka
kwa Nyenza kwa ajili ya kumsaidia katika kesi hiyo ya mirathi.
Alidai
washtakiwa hao katika siku hiyo kwa pamoja walipokea rushwa ya Sh
500,000 kwa ajili ya kumsaidia Agnes Nyenza kwenye kesi yake ya mirathi
iiyopo mbele ya hakimu Omary Mohammed wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni.
Wakili Jacob alidai, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata
hivyo washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na Hakimu Mwijage aliwataka
washtakiwa hao kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya
Sh milioni 10. Washtakiwa hao walikidhi masharti ya dhamana na kesi hiyo
imeahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment