METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 15, 2017

BONGO MOVIE SHINYANGA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI SAKATA LA MADINI KWA KUMPA FILAMU HII FUPI “TANGANYIKA KARNE 18”


Kundi la Uigizaji wa Filamu ‘Bongo Movie Shinyanga’ limempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi hususani madini ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga, Juma Songoro amesema rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania na wazalendo wote.

“Wasanii wa filamu mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kulinda nidhamu na rasilimali za nchi,tunamuombea kila la heri atufikishe tunapopatarajia,tumeandaa filamu hii kama zawadi yetu kwake na na watanzania wote”,amesema Songoro.

Katika kufikisha pongezi hizo,Bongo Movie Shinyanga wameandaa Filamu fupi inaitwa ‘Tanganyika Karne ya 18’ inayoonesha  jinsi nchi za nje zinavyoiba madini ya Tanzania.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com