METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 26, 2017

Asasi ya MARAFIKI CHARITY TZ Wafuturisha watoto Yatima Dar


Vijana wa Marafiki Charity wakipeana majukumu kabla ya kuanza jukumu la kufuturisha watoto hao wa CHAKUWAMA.
Ebby mwenye jezi nyeusi akiwatambulisha baadhi ya vijana wenzake wa Marafiki Charity kwa mmoja wa walezi wa kituo cha CHAKUWAMA wakati walipowasili hapo jana Juni 24.2017 katika tukio hilo la kuwafuturisha watoto hao wanaolelewa kituoni hapo.
  
Baadhi ya wanaumoja wa Marafiki Charity wakiwa kwenye pozi tofauti, akiwemo Devotha, Leah Mushi aliyembeba mtoto Malaika Ebby, Munira Hussen, Esther Namuhisa,na Pendo
 
Omary Mkambara akijadiliana jambo na Naamala katika tukio hilo la kufuturisha
Wakibadilishana mawazo wakati wakisubiria muda
Omary Mkambara akiwajibika katika tukio hilo
Wakisaidia kushusha futari maalum
  
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
   
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
 
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
 
Shughuli ya futari ikiendelea
 
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiendelea kujumuika pamoja katika furai hiyo  maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
 
Marafiki Charity wakiendelea kutoa huduma katika tukio hilo
zoezi la futari likiendelea 
    
Marafiki Charity wakijumuika pamoja katika kupata futari hiyo
 
Omari Mkambara  na Emmanuel Makundi (kulia) wakitoa neno la shukrani kwa kituo hicho
Omary Mkambara akitoa neno la shukrani
Dua maalum kwa ajili ya tukio hilo
Mmoja wa wasimamizi katika kituo hicho akiwatambulisha Marafiki Charity kwa Mama mwanzilishi wa kituo hicho
 
Marafiki Charity wakimsikiliza Mama Mwanzilishi wa kituo hicho wakati walipofika kumjulia hali 
Wakiuliza maswali mbalimbali juu ya kituo hicho cha CHAKUWAMA
 
Mama Mwanzilishi wa kituo cha CHAKUWAMA akiwaombea dua Marafiki Charity 
 
Baadhi ya Marafiki Charity wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza tukio la kufuturisha watoto wa kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA, tukio hilo limefanyika jana Juni 24.2017.

Asasi ya MARAFIKI CHARITY TZ  Wafuturisha watoto Yatima Dar
Asasi isiyo ya Kiserikali ya Marafiki Charity Tanzania ‘Marafiki Charity’,  kwa umoja wao jioni ya jana  Juni 24. 2017, wameweza kujumuika kwa pamoja katika tukio maalum la kufuturisha katika kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA.
Marafiki hao waliweza kuandaa futari hiyo maalum na kwenda kujuika pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha CHAKUWAMA, chenye makazi yake Sinza-Mori (CHAKUWAMA).  
 wakitoa shukrani kwa niaba ya Asasi hiyo ya Marafiki Emmanuel Makundi na Omary  Mkambara walieleza kuwa, moja ya shughuli waliokuwa wamepanga ni kufanikisha tukio hilo la kujumuika pamoja na watoto hao ikiwa ni njia moja wapo ya kutoa sadaka jamii yenye uhitaji.
“Tumeweza kujumuika hapa kwa pamoja tukiwa Marafiki. Hii ni moja ya kuonesha upendo, undugu, uelewano na hutu wetu kwa wenzetu wa kituo hichi cha CHAKUWAMA.” Alieleza Makundi.

Kwa upande wake, Omari Mkambara alieleza kuwa, huo ni mwanzo kwani wamefurahia uwepo wao hapo wa kupata kufuturu pamoja hivyo ikiemo dua walioombewa ni faraja kwa umoja wao huo.

Marafiki Charity ni muunganiko wa marafiki kutoka kada mbalimbali, waandishi wa Habari, wanasheria, wahandisi, wajasiriamali, wahasibu  na watu mbalimbali ambapo wanashirikiana na kwa pamoja katika kusaidia jamii ikiwemo kufanya kazi kwa pamoja za kujitolea, kusaidia wasiojiweza, kubadilishana mawazo na kujumuika pamoja katika mustakabali wa kuijenga Tanzania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com