Na Mwandishi Wetu, Singida
Ni kama ndoto, lakini ni kweli moja ya timu zilizopanda daraja mwaka huu (SINGIDA UNITED FC) imekuja kivingine takribani miongo kadhaaa tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mbali ya maandalizi ya uwanja, basi na usajili wa kocha tishio nchini mholanzi Hans van de pluijm.
Leo majira ya mchana,Singida United Fc wameinasa saini ya mshambuliaji mzoefu aliyeitoa TP MAZEMBE kwa goli pekee mwezi uliopita kwenye michuano ya Club Bingwa Barani Africa si mwingine ni Mzimbabwe *NHIVI SIMBARASHE*
Mshambuliaji huyu wa timu ya Taifa ya Zimbabwe kwa nyakati tofauti na aliyezichezea super sport na Mamelodi Sundowns zote za Africa kusini kwa mafanikio makubwa na baadae kutua Caps United ya Zimbabwe ambayo hadi sasa ndio anamaliza mkataba wake na kuamua kutimukia Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili.
Simbarashe anakuwa mchezaji wa tano wa kimataifa kusajili na Singida United tayari kwa msimu wa VPL 2017/2018.Waliokwisha sajiliwa awali ni wazimbabwe Twafaza Kutinyu,Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Mganda Shafik Batambuze.
Usajili huu unaonesha wazi Singida United hawajaja Ligi Kuu kushiriki bali kutafuta Ubingwa na baadae kwenda kwenye Ligi ya mabingwa barani Africa. Ni hatua nzuri kwa soka la nchi yetu kuona timu ndogo zinafanya mambo makubwa ambayo hayakutarajiwa na wengi,tunawatakia kila raheli Singida United Fc katika maandalizi yao (pre season) yanayoanza pale mwanza tar.12/06/2017.
0 comments:
Post a Comment