Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian
Manoza(Mwenye kofia ya njano0 akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya
Magharibi inayolima pamba ya Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma,
Singida na Tabora walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08)
katika kata ya Mwabusalu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya
wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya
pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian
Manoza amesema Matumizi ya Mbegu bora na Kilimo cha Mkataba
ni suluhu ya wakulima wa pamba inayoweza kuwasaidia kuongeza
uzalishaji.
Manoza ameyasema wakati akitoa taarifa ya Wilaya ya Meatu kuhusu
kilimo cha Pamba kwa Wakuu wa Mikoa nane ya Kanda ya Magharibi inayolima
pamba waliotembelea eneo hilo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera,
Kigoma, Singida na Tabora katika ziara yao kuona mashamba ya uzalishaji wa
mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Amesema kupitia kilimo cha mkataba wananchi watakuwa na
uhakika wa kupata pembejeo bora za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na
viuadudu kutoka kwa watu au makampuni yatakayoweka mikataba nao.
“Tunatarajia kuongeza uzalishaji ili kupata kata nyingi zaidi,
tumewasisitiza wananchi kuwa kilimo hiki cha mbegu bora lazima kiendane na
kilimo cha mikataba, wale wanaohitaji kununua pamba lazima waingie mikataba na
wakulima ili wapate faida walizokuwa hawazipati; baadhi yao wamekuwa
wakihangaika hawana uwezo wa kununua mbegu, viuadudu na kuhudumia mashamba,
lakini wakiingia mikataba hao watakaonunua pamba watatoa huduma zote hizo kwa
wakulima” alisema.
Ameongeza kuwa pamoja na kilimo cha mkataba na matumizi ya
mbegu bora ili kuboresha uzalishaji wa pamba Wataalam wa
Kilimo wanapaswa kuwapa wakulima huduma zote muhimu za ugani ili
wazingatie taratibu zote za kuandaa mashamba, upandaji na utunzaji wa
pamba.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Meja Jenerali Ezekiel Kyunga
ameitaka Bodi ya Pamba nchini kuboresha utaratibu wa kilimo cha mkataba ili
kiweze kuwanufaisha wakulima badala ya kuwakatisha tamaa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri amesema ni
vema Bodi ya Pamba ikaweka utaratibu utakaowawezesha wakulima kupata
mbolea na zana bora za kilimo kwa mkopo ambao watarejesha baada ya
mavuno.
Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga
amesema wakulima wa pamba kwa miaka ya nyuma wamekuwa wanakumbana na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mbegu bora na kutopanda kwa
kuzingatia mistari, hivyo katika msimu wa mwaka 2017 jumla ya tani 8000 za
mbegu bora zitazalishwa kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima na jitihada
zinaendelea kufanywa kupitia kilimo cha mkataba kuhamasisisha wakulima kulima
kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.
Aidha, Mtunga amesema ili kuongeza uzalishaji wa pamba
wakulima wahamasishwe kulima kilimo cha mkataba na ili kilimo cha mkataba
kiwe na tija kwao Bodi hiyo inaendelea kutimiza wajibu
wake kusimamia masharti yaliyowekwa katika utekelezaji wa mikataba
hiyo kati ya wachambuzi na wakulima wa pamba.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi
amesisitiza kuwepo kwa mikakati ya kilimo cha umwagiliaji katika zao la pamba
ikiwepo uchimbaji wa mabwawa makubwa yatakayowasaidia wakulima wakati wote
badala ya kutegemea mvua tu.
Naye Bw.Charles Thobias Mkulima wa kata ya Mwabusalu
ambaye ametumia mbegu bora ya pamba ya (UKM08) amesema mbegu hiyo imekuwa
mkombozi kwa wakulima kwa kuwa kulingana na mazao yalivyo
sasa shambani, mavuno yataongezeka kwa kiasi
kikubwa ikilinganishwa na msimu uliopita.
Utekelezaji wa Mpango wa uzalishaji wa Mbegu bora
katika kata ya Mwabusalu Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu umehusisha
jumla ya wakulima 1,709 katika vijiji vinne ambao kwa pamoja wameweza kulima
jumla ya ekari 6,506 na unafadhiliwa na Programu ya Kuendeleza Kilimo cha Pamba
chini ya usimamizi wa Bodi ya Pamba.
0 comments:
Post a Comment