METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 15, 2017

ZIARA YA MWENYEKITI WA WAZAZI TAIFA MH ALHAAJ BULLEMBO YALETA MATUMAINI CHANYA WILAYA YA CHAMWINO

Na Peter Daffi, Dodoma

Mh Alhaji Bulembo Mwenyekiti wa Wazazi Taifa amekuwa na Ziara kutembelea Wilaya mbali mbaki hapa Nchini, Na Leo Ilikuwa ni Zamu ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Mh Bulembo alifika Chamwino Saa 4 nakukaribishwa kwa Mapikipiki haliyobeba wana CCM waliobeba Bendera za Chama kuanzia Njia panda ya Buigiri mpaka Ofisi ha CCM wilaya ya Chamwino.

M/kiti alisikitishwa na changamoto ya umaliziaji wa Jengo la Ofisi ya Chama ambayo Viongizi wa Chamwino wanatumia kama Ofisi ya Wilaya ingali haijakamilika kwa maana haina Lipu, Dali (ceiling board) Miundombinu ya Maji na Umeme kwa Kifupi Bado haijakamilika, Lakini Viongozi Hawa wa Chama Wilaya Wanaitumia hivo hivo ili Kuendana na Dhana ya Hapa Kazi Tu!

M/kiti wa wazazi Amewachangia Mifuko ya Simenti 40 yenye Thamani ya laki Tano na Elfu ishirini (5,020,000/=)ili Kumalizia Jengo Hilo.

Mbali na Hayo Mwenyekiti Bulembo Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Kuhakikisha anaitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Vitendo Kwa kuhakikisha anatenga Fungu la Asilimia 10 kwa Wakinamama na Vijana Ili Liwe linawafikia kwa Wakati.

Mh Bulembo amefundisha Dhana ya Mtu Mmoja na Cheo Kimoja Ili kuepusha Baadhi ya Watu Kunyimwa haki yao yakikatiba yakuchagua nakuchaguliwa, Amesema Cheo Kimoja nikwa Wenyeviti kuanzia Ngazi ya Matawi mpaka Taifa Hapaswi kuchukua fomu nakuwa kiongozi wa Kisiasa na kisha Kuchukua Fomu Serikalini ya Cheo ambacho Kitahitaji Uwajibikaji wa Cheo hicho kwa Chama au kwa Serikali Mtu huyo atashindwa kufanya kazi vyema kwani Atajikuta analinda Maslahi yake kwa Kupitisha Hoja ama Kugomea hoja kwa maslahi binafsi.

Mh Bulembo Mbali na Hayo amewaasa wana CCM Kupendana nakufanya kazi yakuijenga CCM Mpya na Tanzania Mpya kwa Faida ya Taifa Letu.

Akishukuru M/kiti wa Chama CCM Wilaya ya Chamwino amemuahidi Mh Bulembo Kuwa Pesa alizotoa Zitatumika kwa Makusudio Husika.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com