METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, May 21, 2017

NAIBU KATIBU MKUU UVCCM ZANZIBAR ASHIRIKI UCHAGUZI KATIKA TAWI LAKE

Na Alawi H Foum

Kalenda ya uchaguzi ngazi ya matawi kwa jumuiya zote za CCM ni 18-22/05/2017 ratiba ambayo imepitishwa na mkutano mkuu wa CCM taifa.

Kwa ratiba hiyo leo 21/05/2017 Naibu Katibu Mkuu UVCCM ZANZIBAR Ndg. Abdulghafar Idrissa Juma ametimiza haki yake ya Msingi ya kikatiba kwa kupiga kura yake katika tawi la Kibweni jimbo la Mtoni.

Naibu Katibu Mkuu  mara baada ya kupiga kura na kuchagua viongozi wapya wa jumuiya ambao watakuwa madarakani kwa miaka mitano alipata fursa ya kusema maneno  machache.

"Jana nilikuwa Morogoro kwenye tukio kubwa la mahafali ya wanavyuo ila akili yangu yote ilikuwa Zanzibar nilikuwa nikiwaza ni kwa jinsi gani ningeweza kukamilisha zoezi la kuchagua viongozi wangu wa tawi ambalo Mimi ni mwanachama".

Aidha Ndg. Abdulghafar aliongeza kuwa
"Siku zote sisi viongozi wa juu tulikuwa tunawahamasisha vijana wenzetu wajitokeze kujaza fomu za kugombea ili waweze kuchaguliwa na kuchagua sasa isingekuwa busara kwa sisi wahimizaji kukosa kupiga kura" alisema Abdulghafar.

Naibu Katibu Mkuu  aliwapongeza vijana wote waliofika katika mkutano mkuu huo wa umoja wa vijana tawi la Kibweni na kuwataka wachague viongozi bora na sio bora viongozi kwa maana hao ndio watakaotekeleza dhamira ya jumuiya kuwa kimbilio la vijana jumuiya kuwa ya kisasa inayokwenda na wakati na hatimaye chama kupelekwa kwa wanachama na ndio watakaotegemewa kuhakikisha wanasimamia vema jumuiya ili CCM ishinde kwa kishindo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwisho Ndg. Abdulghafar aliwataka wale wote ambao kura hazijatosha kwa ngazi ya tawi watambue kuwa nafasi zipo nyingi katika ngazi za Kata,Jimbo,Wilaya,Mkoa na Taifa hivyo muda ukifika wajitokeze kwa wingi wajaze nafasi hizo Kaimu Abdulghafar ameridhika na muitikio wa vijana kwa kujitokeza kwa wingi kujaza fomu za kugombea nafasi mbali mbali ngazi ya tawi kwa Chama na Jumuiya kwa ujumla.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com