Gazeti la Mail and Guardian lamfananisha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Trump
Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, imejibu kwa hasira baada
ya gazeti la The mail and Guardian kuchapisha makala inayomfananisha na
rais wa Marekani Donald Trump.
Gazeti la Mail na Guardian limechapisha makala yenye kichwa cha habari "Trump na Zuma wabaya zaidi kuliko waongo."
Ofisi ya Rais inaona kuwa makala hiyo imechapishwa kinyume na "mikataba ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza."
Bunge la Afrika Kusini linafikiria
kupendekeza sheria inayoadhibu lugha ya chuki kwa viongozi wa nchi.
Matusi kwa rais bila shaka itakua ni uhalifu.
Ikumbukwe kwamba Rais Jacob Zuma anakabiliwa na kampeni kadhaa za kumchafua tangu kashfa iliyoitwa "Nkandla" iibuke.
Rais Zuma anashtumiwa hasaa katika chama chake cha ANC, chama tawala nchini Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini alipatikana na
hatia ya kuwa alitumia Euro milioni 20 ya hazina ya Afrika Kusinikwa
kujenga makazi yake binafsi katika eneo la Nkandla.
Alitakiwa kulipa sehemu ya fedha ya fedha hizo.RFI
0 comments:
Post a Comment