Mji wa Mogadishu
Milipuko imesikika katika mji Mkuu wa Mogadishu nchini Somalia usiku wa kuamkia leo.
Kumekuwa na taarifa kuwa mizinga
imelipuliwa karibu na uwanja wa ndege ambapo uchaguzi unatarajiwa
kufanyika, huku wakazi wa eneo la Waberi iliyoko Kusini Magharibi mwa
Mogadishu pia wakithibitisha kusikia milipuko.
Kufikia sasa hakuna maafa au majeruhi
walioripotiwa ingawa hali ya wasiwasi imetanda Mogadishu. Babarabara
zote zimefungwa. Uwanja wa ndege hakuendeki. Na hata wakaaji wengine
hawawezi kuvuka kutoka barabara hii hadi ile.
Mahali pa kufanyia uchaguzi
pamehamishwa, kutoka Chuo cha Polisi hadi Uwanja wa ndege wa Mogadishu
wenye ulinzi mkali. Sababu ya kuongezeka kwa vitisho vya usalama na
rushwa .
Hii leo Ndege hazitaruhusiwa kutua au kupaa kutokea uwanja huu, kwa kuwa ni siku ya kupiga kura.
Mfumo wa uchaguzi nchini Somalia
umeharibika kama ilivyo miundombinu yake. Haina daftari la wapiga kura.
Wabunge mia tatu na ishirini na tisa ndio watakaomchagua Rais ajaye.
Lakini sasa tuhuma za rushwa zinatishia kuvuruga mchakato mzima. Kuna
tuhuma nzito kuwa wabunge wengi wamelipwa mamilioni ya dola kushawishi
upiga-kura wao.
Uchaguzi wa Urais,Somalia
Wanawake wengi zaidi watashiriki kupiga
kura wakati huu, hivyo kufanya asilimia ishirini na sita ya kura zote za
bunge. Ingawa wanawake wawili waliotangaza nia ya kuwania Urais akiwemo
Fatuma Dayyib aliyetangazwa sana, walijitoa.
Licha ya maswali mengi kuhusu uchaguzi
huu, wananchi wa Somalia wanatumai kuwa kufanikiwa kwa uchaguzi huu
utawaongoza kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020. Lakini kwanza, nchi
inahitaji Rais na serikali inayofanya kazi.BBC
0 comments:
Post a Comment