METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 31, 2017

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MWAKA 2017 AWEKA JIWE LA MSINGI WA KITUO CHA POLISI CHA KATI - KATA YA KIBAMBA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg Amour Hamad Amour ameweka Jiwe la Msingi wa Kituo Cha Polisi Cha Kati-Kata ya Kibamba, Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam.

Mwaka 2016 wananchi wa mtaa wa Gogoni kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa waliamua kujenga kituo cha polisi cha kati  kwa kutumia mguvu za wananchi na wadau mbalimbali waliopo nje ya mtaa kutokana na kukithiri kwa uhalifu katika mtaa ambapo wananchi wamekwisha changia jumla ya Tsh. 53,000,000/ = na NSSF imechangia Tsh. 50,000,000/= sawa na jumla ya Tsh. 103,000,000/=.

Eneo la ujenzi kituo cha polisi lina ukubwa wa ekari  moja (1). Jengo la kituo cha polisi linakusudiwa kuwa na vyumba 13, vyumba vitatu ni kwa ajili ya maabusu ya wanaume,wanawake na watoto zenye vyoo vya ndani, vyumba vya ofisi na vyoo 4.

kituo hicho cha polisi Gogoni kikimalizika na kufunguliwa kitapunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa katika mtaa, kata na Wilaya ya Ubungo kwa ujumla.

Changamoto zilizopo katika umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha polisi ni upatikanaji wa Tshs. 190,000,000/= zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.

Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com