METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 25, 2017

WATENDAJI MANISPAA YA KIGAMBONI WAPONGEZWA

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza watendaji wa Manispaa ya Kigamboni kwa moyo wao wa kujituma katika kuitumikia manispaa hiyo mpya.

Jafo ametoa pongezi hizo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kuzungumza na watumishi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa mabweni, madarasa, maabara na vyoo katika shule ya sekondari ya Somangira ambapo serikali ilipeleka sh. milioni 259 ili kujengwa miundombinu hiyo na kufanya shule iwe na uwezo wa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano waliochaguliwa kwa awamu ya pili.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea hospitali ya Vijibweni na kuwamwagia sifa watendaji wote wa hospitali hiyo kwa usimamizi mzuri kwa kuwa na mazingira ya usafi wa kuvutia.

Hata hivyo Jafo alielekeza kutenga eneo Maalum kwa ajili ya duka Maalum la wagonjwa wa bima ya afya ili wagonjwa wote wa bima wasikose dawa wanapofika hospitalini kupata matibabu.

Naibu Waziri huyo pia amempongeza Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi wote wa wilayani kwa kazi nzuri ya usimamizi wa wilaya hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miradi ya wilaya ya Kigamboni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa sekta ya afya wilaya ya Kigamboni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitembelea Hospitali ya Vijibweni wilaya ya Kigamboni.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua maabara na madarasa katika sekondari Somangira.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua maabara na madarasa katika sekondari Somangira.
Bweni la wasichana lililokamilika kujengwa katika sekondari ya Somangira.
Watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Wanafunzi wa sekondari ya Somangira wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea shuleni hapo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com