Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2017 Amour Hamad Amour amezindua Jengo la Kituo Cha Huduna kwa Wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika kituo Cha afya Mbezi.
Akizungumza mara baada ya kufungua jengo Hilo Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge Ndg Amour Hamad Amor ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo sambamba na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwa maandalizi bora ya Mbio za Mwenge kuliko maeneo mengine yote ulikofika Mwenge huo.
Alisema kuwa Juhudi za serikali ni kuimarisha huduma bora za afya kwa wananchi hivyo jengo Hilo litatoa fursa kwa wananchi kupata huduma karibu na maeneo wanayoishi.
Amour amewashauri wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupatiwa ushauri nasaha sambamba na kutoa wito kwa madaktari kutoa huduma bora kwa wananchi pasina unyanyapaa.
Jengo la kituo cha huduma kwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi (CTC) katika kata ya Mbezi uliibuliwa na idara ya Afya Manispaa ya Ubungo mwaka 2017 kwa kuhakikisha watu wanaoishi na VVU wanapewa huduma karibu na wanapoishi.
Mradi huo unatajwa kuwa mkombozi mkuu katika jimbo la Kibamba ambalo lina jumla ya kata 4. Ambapo kata nyingi zilizoko pembezoni wa Manispaa ya Ubungo zitaweza kupata huduma za wanaoishi na VVU maana walikuwa wanaenda maeneo ya mbali kupata huduma hii.
Jengo hilo lina vyumba 8 na vyoo 2 ambapo mchanganuo wake ni chumba 1 cha Daktari, chumba cha taarifa(data room),chumba cha kuchukulia sampuli (Phlebotomy),chumba cha Stoo,chumba cha Dawa(pharmacy),chumba cha Ushauri Nasaha (counseling room),chumba cha Daktari Mfawidhi na chumba cha Muuguzi.
Mradi huo utasaidia wagonjwa wanaoishi na VVU na wanaoutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV) 1672 katika kituo cha Afya Mbezi.
Mradi pia unategemewa kuhudumia zaidi watu wapatao elfu ( 10,000) wastani wa wagonjwa wengine wa kawaida wanaokadiriwa kuwa 50 wanaozuru kila siku kuhudumiwa wakiwemo wale wanaotoka nje ya kata ya Mbezi na maeneo ya karibu na mitaa iliyo mbali kama Msumi, Msakuzi na Mpiji Magoe.
Vile vile jengo hilo ni la kisasa na rafiki kwa wagonjwa na watoa huduma na kuleta ufanisi mkubwa kuliko ilivyokuwa hapo zamani. Jengo hili limegharimu kiasi cha Tshs 125 milioni ambazo zimetolewa na wafadhili ambao ni MDH (Management and Development for Health).
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mganga mkuu wa Wilaya ya Ubungo
0 comments:
Post a Comment