Nguruwe wawili mbele ya Bunge la Uganda, mjini Kampala, Juni 17 2014.
Alhamisi
hii nchini Uganda, wanaharakati wamepeleka nguruwe mbele ya Bunge la
Uganda katika mji mkuu, Kampala, kupinga dhidi ya uamuzi uliyopitishwa
wa kufidia wabunge nchini humo.
Ilibainika wiki hii kwamba fedha zilizotengwa katika bajeti ya taasisi hiyo ili kufidia gharama za mazishi kwa wabunge.
Takriban Dola elfu kumi na tano zimetengwa kwa kila mazishi.
Baadhi ya wabunge wametetea mpango huo.
Baadhi ya
wabunge wamesema kwamba huduma ya mazishi ya askari waliokufa
wakilihudumia taifa yanalipwa na serikali na kwamba wabunge wanapaswa
kuewa huduma kama hiyo.
Bunge
nchini Uganda linatarajiwa kutumia Dola za Marekani 177,000 kuwatuza
medali wabunge 1,200 waliohudumu katika bunge la nchi hiyo kati ya mwaka
1962 hadi 2012.
Vyombo
vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa sherehe za kuwatuza wabunge hao
zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika maadhimisho ya miaka 50 ya
Bunge hilo.
Hatua hii
imekuja baada ya Gazeti la serikali ya New Vision kutangaza kuwa bunge
limepanga kutumia fedha hizo kufanikisha shughuli hiyo.
Hata
hivyo raia wa Uganda, wameonekana wakipinga matumizi ya fedha hizo
katika sherehe hizo wakati huu raia wa nchi hiyo wakiendelea kukabiliana
na hali ngumu ya kiuchumi.
Wabunge 13 wamefariki dunia kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
RFI
0 comments:
Post a Comment