Na Ofisi ya Mbunge, Ilemela
Halmashauri nchini zimetakiwa kutoa mikopo na ujuzi kwa vikundi vya kina mama na vijana ili kupunguza changamoto ya ajira na kufikia lengo la Serikali la Tanzania ya Viwanda kunakoambatana na kumpunguzia mzigo mzito mwanamke
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika kongamano la siku ya mama lililojulikana kama Nyota Forum liliandaliwa na Kampuni ya Sahara Media likiwa na Kauli Mbiu ya ‘ Heshima kwa Mama ’lililofanyika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali, wanasheria , wanaharakati na wataalamu wa mambo ya jinsia na wanawake likipambwa na burudani kutoka kwa wasanii tofauti tofauti nchini ambapo amesema
‘ Natoa wito kwa atendaji wa Halmashauri zote nchini kutoa mikopo na ujuzi kwa makundi ya kina mama na vijana hii itasaidia kupunguza changamoto ya ajira, itasaidia upatikanaji wa kodi kwa Serikali kwasababu watu wake watakuwa wanazalisha lakini ndo uelekeo wetu kama nchi ya viwanda kunakoenda sambamba na kumpunguzia mzigo mwanamke ’ alisema
Aidha Dkt Mabula amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha inamkomboa mwanamke ikiwemo mafunzo na mikopovilivyoanza kutolewa huku akiasa uzingatiaji wa afya katika kupanga familia
Akimkaribisha mgeni rasmi meneja wa Kiss Fm Bi Sharobano Abubakar amemshukuru mgeni rasmi kwa kukubali kuhudhuria Tamasha hilo pamoja na majukumu ya kitaifa aliyonayo huku akifafanua lengo kuu la tamasha hilo ambapo amesema ‘ Napenda kuwajuza kuwa lengo kuu la tamasha hili la Nyota Forum 2017 ni kuibuamajukumu ya kina mama, kujua thamani ya mama, changamoto zinazomkabili na kuzitafutia suluhu yake ’
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
14.05.2017
0 comments:
Post a Comment