METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 16, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AWATUNUKU WADAU WA SOKA VYETI VYA SHUKRANI

Na Ofisi Ya Mbunge

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mandeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewatunuku wadau mbalimbali wa soka waliokuwa wanaisaidia timu ya mpira wa miguu ya wanawake ya mkoani Mwanza ijulikanayo kama Marsh Queens  ikiwa ni jitihada za kutambua na kuthamini mchango wao katika kukuza michezo nchini

Akizungumza katika  hafla hiyo iliyojumuisha wadau wa soka, viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla huku ikitanguliwa na harambee ya kuichangia fedha timu hiyo Dkt Mabula amesema kuwa serikali itaendelea kuvisaidia virabu mbalimbali vya michezo nchini huku akitakawadau wengine kuzidi kujitokeza katika kuisaidia timu hiyo iweze kufanya vizuri zaidi
‘…Serikali ipo pamoja nanyi na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali lakini na sisi sote  tunaowajibu wa kuwatia moyo, kuwatembelea, kuwasaidia huku tukiweka mikakati ya dhati ya kuhakikisha tunafanikiwa zaidi nitumie jukwaa hili kuwaomba wadau wengine kuendelea kusaidia …’ Alisema

Aidha Dkt Mabula ameitaka Timu hiyo kuongeza juhudi ili kutia moyo na chachu kwa wadau wote ili kuendelea kuisaidia

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe Marry Tesha akimkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa timu ya Marsh Queens itaendelea kutoa shukran kwa namna moja au nyengine kwa namna Mhe Mabula na wadau wengine wanavyoisaidia kutoka awali mpaka sasa huku akiongeza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya kuonyesha kwa vitendo shukrani zao za dhati kwa wadau wote wa soka wanaounga mkono timu hiyo

Akihitimisha  hafla hiyo Katibu wa Timu ya Marsh Academy Ahmad Azizi mbali na kumshukuru Mbunge wa Ilemela kwa namna  anavyojitoa kuisaidia jamii pamoja na majukumu ya kitaifa aliyonayo amemuhakikishia kuwa Timu yake itaendelea na jitihada za kuhakikisha inafanya maajabu katika mchezo wa soka kwa kufanya vizuri zaidi

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ‘

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
14.05.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com