METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

UVCCM ZANZIBAR YAENDELEA KUTIMIZA AHADI

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

UVCCM ZANZIBAR imeendelea kutimiza ahadi zake mbali mbali ilizoweka wakati wa ziara ya Kaimu Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Nd Abdulghafar Idirissa.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kutoka Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba Ndg Abdalaah Mohd (kidishi) jana alikabidhi mifuko ishirini (20) ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tatu na alfu kumi (310,000) mifuko hiyo 20 kwa niaba ya Kaimu Naibu Katibu Mkuu UVCCM ZNZ ikiwa ni ahadi ambayo aliitoa 02/03/2017 Alipokuwa ziarani Pemba wilaya ya mkoani Tawi la Mkungu.

Ndg Abdulghafar Idirissa Juma Kaimu Naibu UVCCM ZNZ alipokuwa akikaguwa utekelezaji wa ilani na agizo la Mwenyekiti wa Chama Taifa kutaka chama kipelekwe kwa wanachama alipofika tawi la Mkungu alikagua ujenzi wa tawi hilo jipya ambao uliazishwa kwa nguvu na michango ya vijana wa CCM.  Baada ya kuona hatuwa nzuri iliyofikiwa nae akaahidi kutoa mifuko 20 ya saruji kama mchango wa UVCCM kusaidia katika ujenzi huo.

Ndg Abdallah (MNEC) wakati akikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Naibu wa UVCCM ZNZ alimpongeza sana Naibu kwa kuwa muungwana hasa baada ya kuahidi na kutekeleza ahadi yake kwa ukamilifu na kwa wakati.

"CCM ikipata viongozi bora kama hawa wanaojuwa shida za wanaowaongoza na kuzitatuwa haitaondoka madarakani milele, binafsi nitowe wito kwa viongozi wengine tuige mwenendo wa Naibu wa vijana tukiwaahidi wenzetu tusiwakimbie turudi kutekeleza tulichowaahidi" alisema Mhe Abdalah.

Nae Katibu UVCCM Wilaya ya Mkoani Pemba Nd MOHD aliwataka viongozi wa chama wa tawi hilo la Mkungu kuwa karibu na uongozi wa UVCCM wa tawi  hilo kwa kuwapa mashirikiano ya kutosha wanapotaka kufanya jambo la kukijenga chama hasa ukizingatia wao ndio walezi.

Katibu UVCCM Wilaya ya Mkoani alisema alichokifanya Naibu ni kitendo cha kupongezwa maana kimetengeza heshima kwa UVCCM wilaya ya Mkoani.

Mwenyekiti wa CCM Tawi hilo la Mkungu Alipokea saruji hiyo na  kuwataka vijana waitumie saruji hiyo kwa malengo yaliyo kusudiwa na kuwakumbusha kuwa kipindi walicho nacho ni mvuwa sio kipindi rafiki kwa saruji waitumie haraka kukamilisha ujezi wa tawi hilo pia aliwakumbusha vijana kuwa sasa ni wakati wa uchaguzi wajitokeze kwa  wingi kuchukuwa fomu za uongozi wa chama na jumuiya zake.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com