METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

MANISPAA YA IRINGA KUJENGA KITUO CHA SOBER HOUSE: JOSEPH LYATA NAIBU MEYA

Naibu meya wa halmashuri ya manispaa ya iringa Joseph Nzala Lyata akiwa na kamati ya ukimwi ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwenye ziara ya kuitembelea kituo cha Iringa sober house kilochopo Kata ya Kihesa.Naibu meya wa halmashuri ya manispaa ya iringa Joseph Nzala Lyata akiwa na kamati ya ukimwi ya Manispaa ya Iringa wakisikiza maelezo kutoka kwa viongozi wa Iringa sober house


Na Fredy Mgunda, Iringa

Kutokana na kuwepo kwa wananchi wanatumia ya madawa ya kulevya  katika halmashauri ya manispaa ya iringa wameamua kutenga eneo kwa kujenga majengo ya kuwatibu waathirika wa madawa ya kulevya(SOBER HOUSE)  ili kuiokoa jamii inayotumia madawa ya kulevya.

Akizungumza na blog hii naibu meya wa halmashuri ya manispaa ya iringa Joseph Nzala Lyata alisema kuwa wamebaini kuwa kuna baadhi ya kataza manispaa ya iringa ambazo zinaongoza kuwa na watumiaji wengi wa madawa ya kulevya mfano kata ya kitanzini miomboni,ipogolo,mwangata na kihesa.

Hivyo kutokana na hilo tumeamua kuanza kuandaa eneo maalum kwa ajili ya kuwa kujenga majengo ya sober house ndani ya manispaa ya iringa na kuongeza kuwa kamati ya ukimwi ilitembelea kituo cha IRINGA SOBER HOUSE kwenda kujifunza nini kinafanyika katika kituo hicho.

“Tumekuja na kamati ya ukimwi ikiongozwa na mimi mwenye ambaye ni mwenyekiti tumekuja hapa kujua mambo mengi lakini tumejifunza kuwa manispaa ya iringa inawaathirika wengi lakini kukosekana kwa majengo ya kuishi waathirika wa madawa ya kulevya kunaifanya jamii kukosa huduma hiyo”alisema Lyata

Lyata alisema kuwa ameongea na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya iringa ili kutafuta njia za kulimaliza tatizo hili la matumizi ya madawa ya kulevya kwa kushirikiana na sekta mbalimbali ambazo zinahusika kwa umoja katika kukabiariana na tatizo hilo.

Manispaa ya iringa ni lazima tutafute njia mbadara ya kumaliza tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya kwa kuwa matumizi ya madawa yanaongeza maambukizi ya ukimwi hivyo lazima tufanye kazi zote mbili ili kuwaweka wananchi wa manispaa ya iringa kuwa salama na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na maambukizi ya ukimwi.

Kamati ya ukimwi manispaa ya Iringa imejipanga kutoa elimu ya maambukizi ya ukimwi kuanzia ngazi ya mitaa,kanisani,misikitini,kata na viongozi mbalimbali kutoka serikalini na taasisi mbalimbali ambazo sio za kiserikali lengo likiwa kila mtu afikiwe na elimu ili kumaliza kabisa tatizo la matumizi ya madwa ya kulevya pamoja maambukizi ya ukimwi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com