Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Urio akiwa
amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha
Chakuwama kilichopo Sinza wakati wa hafla fupi ya kutoa msaada
iliyofanyika Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Kituo hicho, Hassan Hamisi (kulia), akitoa historia fupi ya kituo hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakiwa wamewabeba watoto katika hafla hiyo.
Mfanyakazi bora wa benki hiyo, kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba, Amani Mgweno akishiriki kubeba zawadi za watoto hao.
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kushoto), akishiriki kutelemsha zawadi hizo kutoka kwenye gari. (P.T)
Zawadi zikiendelea kutelemshwa.
Zawadi
zikitelemshwa. Kulia ni mtoto wa mfanyakzi wa benki hiyo, Asha Mayuva,
akionesha upendo kwa watoto wenzake kwa kuwapelekea zawadi.
Wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa wamewabeba watoto mapacha wanaolelewa katika kituo hicho.
Zawadi
zikipangwa. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Seka Urio, Asha
Mayuva, Raphael Mlute na Magreth Lwiva. ' Hapa ni Kazi Tu kwa kwenda'
Taswira
ya keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ' Hakika NMB Tawi la Mlimani
City mmeonesha upendo wa hali ya juu kwa watoto hao barikiweni sanaaa'
Mwonekano wa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na watoto hao.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa kwenye hafla hiyo fupi.
Hapa ni furaha tupu.
Hapa ni nani kama baba?
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ikikatwa.
Hapa ndipo unapoweza kuutambua utamu wa keki.
"Hapa ni kama wanafikiria sijui tuondoke na mtoto huyu"
Na Dotto Mwaibale
BENKI
ya NMB Tawi la Mlimani City imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Makao
ya Kulea Watoto Yatima ya Chakuwama yaliyopo Sinza jijini Dar es Salaam
ikiwa ni moja ya njia ya kujumuika na jamii inayo wazunguka.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo
ambao ni vyakula na vifaa vya shule kwa ajili ya wanafunzi Meneja wa
benki hiyo wa tawi hilo, Seka Urio alisema ni kawaida kwa benki hiyo
kushiriki shughuli za kijamii na kutoa faida wanayoipata kwa wananchi
ambao ndio wateja wao.
"Tunajisikia
faraja kutoa vitu vichache kwa watoto wetu ambao mnawalea katika kituo
hiki pia ni kurudisha faida tunayoipata kwa jamii" alisema Urio.
Urio alisema vitabu vyote vya dini vinaelekeza kuwajali na kuwafariji wenzetu wenye uhitaji ikiwa ni agizo lake mwenyezi mungu.
Katibu
wa Kituo hicho, Hassan Hamisi alisema kituo hicho chenye watoto 60,000
wakike wakiwa 25 na kiume 35 tangu kianzishwe kwake mwaka 1998 kimepata
mafanikio ya kupata nyumba yao ya kuishi watoto hao, malezi huduma za
elimu na afya.
"Kwa
kweli tukiangalia tulipoanzisha kituo hiki na sasa tumepiga hatua licha
ya kuwepo changamoto kwani tunasomesha watoto katika shule mbalimbali
za sekondari na msingi na wengine wapo vyuo vikuu ni jambo la kujivunia"
alisema Hamisi.
Alisema
watoto wengine wamepata kazi baada ya kuhitimu elimu katika ngazi
mbalimbali na baadhi yao wameoa na kuolewa na sasa wanaendesha familia
zao.
Hamisi
alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuanzisha utaratibu wa wanafunzi
kupata elimu bure kwani umewapunguzia changamoto ya kuwalipa ada
wanafunzi 47 wanao walea katika kituo hicho.
Hamisi
alisema pamoja na kupiga hatua bado wanachangamoto mbalimbali kama
chakula na nyumba kwani kila siku watoto wamekuwa wakiongeza katika
kituo hicho kutokana na migogoro ya kifamilia, wazazi au walezi kufariki
na kuwaacha watoto na watoto kutelekezwa hivyo akawaomba wadau wengine
wajitokeze kuwasaidia kama ilivyofanya benki hiyo.
Hafla
hiyo ilihudhuria na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo waliwafariji
watoto yatima kwa kuwapa vitu mbalimbali na kuzungumza nao ambapo
waliwasisitizia kuzingatia masomo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments:
Post a Comment