METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 10, 2017

TBL Group Kidedea Tena Tuzo Ya Rais Ya Mzalishaji Bora 2016!

A
Makamu wa Rais,Mh.  Samia Suluhu Hassan  akimsikiliza kwa makini  Mwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa TBL Group   Deogratius  ( wa pili kushoto) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo  wakati   wakati wa utoaji wa  Tuzo za Rais za  mzalishaji bora wa Viwanda  kwa mwaka 2016 katika hoteli ya Serena mwishoni  mwa wiki.Kulia ni Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji  Charles Mwijage na kushoto ni Afisa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi.
A 1
Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimkabidhi  Tuzo ya mshindi wa jumla ya mzalishaji bora wa viwanda mwaka 2016   Mwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa TBL Group  Deois  Deogratius  wakati wa hafla tuzo hizo  iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI)  na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
A 2
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimkabidhi  Tuzo ya mshindi  ya  mzalishaji bora wa viwanda mwaka 2016   Meneja wa  Kiwanda cha  TBL  jijini Dar es Salaam,Calvin Martin,  wakati wa hafla tuzo hizo iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania( CTI)  jijini Dar es salaam.
A 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Samia Suluhu Samia akionyeshwa moja ya chupa za konyagi katika vifungashio vya kisasa  .  
A 4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Samia Suluhu Hassan akingalia bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya TBL Group
A 5
 Meneja wa bia ya asili ya Chibuka Super  inachozalishwa na TBL Group , Fredy Kazindogo (kushoto) akimuonyesha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan chupa ya Chibuku iliyotengenezwa kwa ubora  wakati banda la TBL Group.
A 7
A 8
Wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kampuni yao kuibuka kidedea.

Kampuni ya TBL Group imeibuka tena na ushindi wa jumla wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa mwaka 2016.Imefanikiwa kuweka rekodi ya mwendelezo ya ushindi ambapo pia mwaka jana iliibuka kuwa mshindi wa jumla wa tuzo hii.

Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki  ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Mh.Samia Suluhu Hassan.

Mh.Samia Suluhu Hassan, aliahidi kuwa serikali itazifanyia kazi haraka changamoto zinazokabili wafanyabiashara wenye viwanda ili kufanikisha dhamira yake ya kujenga Tanzania ya Viwanda.

TBL ni kampuni ya kwanza kutengeneza vinywaji vyenye kilevi nchini.Mbali na tuzo ya mzalishaji bora inashikilia pia rekodi ya tuzo ya mwajiri bora nchini. Mafanikio haya yanatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye mifumo ya uzalishaji,raslimali watu na kunufaisha jamii  kupitia mzunguko wa biashara zake ambao umefanikisha kupatika ajira zipatazo 2,000  za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja .

 Kampuni pia imekuwa mstari wa mbele  kuchangia maendeleo ya taifa kupitia kulipa na kukusanya kodi za serikali ambapo pia inashikilia tuzo mbalimbali kwa kuwa mlipa kodi bora nchini.

Mbali na kushinda Tuzo ya mzalishaji bora kwa mwaka huu pia imefanikiwa kutunukiwa tuzo ya kuwa kiwanda bora cha vinywaji nchini na tuzo ya matumizi mazuri ya nishati katika mchakato wa uzalishaji-Tuzo hizi zinazidi kudhihirisha umakini wa TBL Group katika uwekezaji wake ambapo pia inashikilia tuzo ya kimataifa ya mwajiri bora iliyotunikiwa mwaka jana na taasisi ya Top Employers’ Institute yenye makao yake makuu nchini Uholanzi kutokana na kuwa miongoni mwa makampuni yanayozingatia  kanuni bora za raslimali watu katika viwanda vyake duniani.

Akiongea baada ya hafla ya kupokea tuzo,Meneja wa kampuni ya TDL ambayo iko chini ya TBL Group,Devis Deogratius alisema “Ushindi huu wa TBL mfululizo unadhihirisha kuwa Tanzania ya Viwanda bora inawezekana na mbali na ushindi huu viwanda vyetu vya bia vya Mwanza, Mbeya, Arusha na  Dar es Salaam vinashikilia rekodi ya kushinda tuzo za kuwa miongoni mwa viwanda bora barani Afrika na duniani.”

Deogratius alisema kipaumbele kikuu ambacho kampuni inazingatia ni kuhakikisha inazalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kwa upande wa vinywaji vyenye kilevi imekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii juu ya unywaji wa kistaarabu na ni miongoni mwa makampuni  yanayotekeleza maazimio ya mkutano wa kidunia wa watendaji wakuu wa makampuni yanayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kuhusiana na kutoa elimu ya Unywaji wa kistaarabu kwa watumiaji wa vinywaji vyenye kilevi.

Mafanikio haya yote yanaifanya TBL kuendelea kuaminika kwa wengi kama kampuni halisi  ya kitanzania inayotengeneza bia bora kwa kutumia malighafi kutoka nchini ambazo licha ya kupendwa na wananchi wengi zinakubalika kwenye masoko ya nje na zimetunikiwa tuzo mbalimbali za kimataifa za ubora.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com