Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni
ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akizungumza Makao Makuu ya
Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakati wa
hafla ya kuwaaga vijana wanne wa kitanzania ambao wanakwenda nchini
India kwa mafunzo ya miezi tisa ya kutengeneza magari. Kutoka kushoto ni
viongozi wa kampuni hiyo, Sarvan Keshri na Udayagiri Veeru.
Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akisisitiza jambo.
Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga
vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi
akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni mmoja wa viongozi wa
kampuni ya Tata, Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa
Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Viongozi wa kampuni hiyo ukitoa zawadi
ya ua kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi katika hafla fupi ya
kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi (kulia),
akikabidhiwa zawadi ya picha ya tembo na viongozi wa kampuni
hiyo. Kutoka kushoto ni Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa
Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
Mama wa msichana pekee anayekwenda
kupata mafunzo hayo, Fatma Mussa Ngulangwa (kushoto), akimkabidhi binti
yake, Mariam Shamte maua ikiwa ni ishara ya kumuaga.
Fr.Lucas Wakuganda akimkabishi maua mtoto wake anayeondoka kwenda masomoni nchini humo.
Mhitimu wa mafunzo hayo, Osmund Kapinga (katikati), akiwa amewainua mikono vijana hao ikiwa ishara ya kuwaaga.
Mkufunzi wa mafunzo wa kampuni hiyo,
Oscar Mwakagenda (kushoto), akitoa maelekezo ya injini za gari
zinazofanya kazi mbele ya mgeni rasmi na uongozi wa kampuni hiyo.
Ni furaha tupu katika hafla hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya karakana ya mafunzo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Tata imetoa ufadhili kwa vijana wanne wa kitanzania kwenda nchini India kujifunza utengenezaji wa magari.
Kati ya vijana hao msichana ni mmoja
ambapo wanatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea mji wa Jamshedpur
nchini humo kwa mafunzo ya miezi tisa kupitia mpango wa Skill pro-
International Business Commarcial Vehicles Skill Development Program.
Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga
vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi akizungumza
Dar e Salaam jana aliwataka vijana hao wakiwa nchini humo kuwa mabalozi
wa kutangaza sifa nzuri ya Tanzania na si vinginevyo.
“Tumieni fursa hii mliyoipata kwenda
kusoma na kuitangaza nchi yetu msiende kucheza na kututia aibu kwani
katika vijana 25 kutoka nchi mbalimbali za Afrika nyie wanne ndio
mnaiwakilisha nchi yetu” alisema Masingi.
Masingi aliishukuru kampuni hiyo kwa
kuwawezesha vijana hao na kuahadi serikali kushirikiana nayo ili kupanua
soko la ajira kwa vijana nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya
Tata Tanzania Prashant Shukla alisema hii ni awamu ya tatu kwa kampuni
hiyo kupeleka vijana nchini India kujifunza kutengeneza magari ambapo
kwa awamu ya kwanza hakuna kijana wa kitanzania aliyehudhuria mafunzo
hayo.
Alisema kwa awamu ya pili alipelekwa
mtanzania Osmund Kapinga ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi bora na katika
awamu hii ya tatu wanakwenda hao wanne.
Alisema lengo la kuwapeleka vijana hao
nchini India ni kujifunza kazi hiyo ili nao wakirudi waweze kuwa walimu
wa wenzao hivyo kuisaidia serikali kukuza ajira nchini hasa kwa vijana.
Alisema kampuni hiyo kwa Tanzania
inafanya kazi mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza lakini
wanatarajia kwenda mkoani Mbeya kufungua tawi na baadae itafuatia mikoa
mingine ambapo vijana wanaopata mafunzo kupitia mpango huo wataenda
kuwafundisha wenzao.
Mhitimu wa mafunzo hayo nchini humo
Osmund Kapinga alisema kampuni hiyo ni kubwa na mbali ya kutengeneza
magari ya aina zote inavitu vingi inavyo tengeneza hivyo aliwasihi
wenzake wanaoondoka kuchangamkia fursa hiyo hadimu ili wakirudi waweze
kuwasaidia watanzania wenzao.
Vijana waliopata fursa ya kwenda kupata
mafunzo hayo ni Mariam Hemed Shamte, Anord Peter Nditu, Elias Jones
Tette na Adam Abdallah Pwimu.
0 comments:
Post a Comment