METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, June 22, 2023

MKOA WA PWANI WANG'ARA WANAWAKE WAINUKA NA KIWANDA CHA VIFUNGASHIO



Na Saida Issa, Dodoma 

SERIKALI imesema kuwa Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa Mikoa iliyofanya vizuri katika kuanzisha majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo, Jukwaa la Mkoa limeanzishwa kwa mafanikio makubwa hadi kufikia wazo la kuanzisha kiwanda cha vifungashio. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na Makundi maalum Mwanaidi Ali khamis alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vitimaalumu Pwani Subiri Mgalu alipouliza 
Je, Serikali ina mpango gani wa kuyapatia mafunzo majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika ngazi za Vitongoji, Vijiji, Kata na Wilaya Mkoani Pwani? 

Wizara katika bajeti yake ya mwaka 2023/24 imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 161 kwa ajili ya kujenga uwezo wa majukwaa ambapo Mkoa wa Pwani utakuwa miongoni mwa Mikoa itakayohusika. 
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com