Wananchi wa Ipogolo wakitoa malalamiko yao |
Mwananchi akitoa malalamiko yake |
Badhi ya wananchi waliotakiwa kuondoka |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kulia akiwataka wananchi kulinda mazingira |
Hivi ndivyo mazingira yalivyoharibiwa mlima wa Ipogolo |
kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa ikiwa eneo la Ipogolo |
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kulia akiwa na mtendaji wa kata ya kitanzini |
Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa mkoa wa
Iringa amemtaka afisa mtendaji wa kata
ya Kitanzini katika Halmashauri ya
wilaya ya Iringa kujisalimisha
kituo cha polisi baada ya kukiuka
agizo la makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan la utunzaji wa mazingira mlima wa Ipogolo.
Hatua ya mkuu
huyo wa mkoa kuagiza
mtendaji huyo kuchukuliwa hatu kali
imekuja baada ya kuruhusu wananchi wafanyabiashara ndogo ndogo kuvamia msitu wa hifadhi ya milima ya Ipogolo kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara kama ambavyo jana mtandao wa matukiodaimaBlog ulivyoibua taarifa hii .
Akizungumza leo eneo
la soko la magari mabovu baada ya
kufanya ziara ya ghafla
eneo hilo kushuhudia
uharibifu huo ,mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa amesikitishwa na hatua ya wafanyabiashara hao kufyeka
miti ya asili kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara .
Hivyo alisema kuwa hawezi
kukubali uharibifu huo wa mazingira kufanyika katika eneo hilo na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa na kuwataka wananchi kuturubuniwa na watendaji kuingia maeneo ya hifadhi.
Alisema kuwa Pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo
wa mashine tatu kuhamishiwa eneo la
soko la magari mabovu ila haina maana
kwao kuvamia mlima na kuharibu
mazingira kwa kutaka kujenga
vibanda vya biashara .
“ Eneo lililotengwa kwa
ajili ya wafanyabiashara lipo
hivyo hakuna sababu ya kuharibu mazingira tumewatengea eneo
la kufanyia biashara na isipo tosha hapa ngome
kuna soko ambalo hadi leo halitumiki ipasavyo na ni eneo kubwa kwa hili namuagiza mtendaji wa kata aliyehusika
kugawa mlima huu afike mwenyewe
polisi ili achukuliwe hatua kali “
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameagiza uongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
kusimamia zoezi la upandaji wa
miti katika eneo hilo ili
kurudisha hadhi ya mazingira hayo
.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela alisema kuwa
atasimamia agizo hilo la mkuu
wa mkoa na kuwataja wananchi wanaoendelea kujenga eneo hilo kusitisha na kuwa mgambo wa manispaa ya Iringa
wataendelea kulinda eneo hilo .
Wakizungumzia
hatua hiyo iliyochukuliwa na mkuu
wa mkoa wa Iringa baadhi ya
wafanyabiashara hao walisema
kuwa mbli ya mtendaji huyo kuchukuliwa hatua bado anapaswa kurejesha gharama zao walizotumia kufanya maandalizi ya
ujenzi huo .
Kwani walisema wao
wasingefika kujenga eneo hilo bila kuelekezwa na viongozi wa
serikali na kuwa ujenzi huo umeanza wiki
mbili kabla na serikali ya Halmashauri
ya wilaya ilikuwa ikiona
alisema Anitha Luhavi .
Wakati John Sanga alisema
kuwa kabla ya kupewa
eneo hilo walikuwa
wakitoa pesa kwa mtendaji
wa mtaa huo ambae alikuwa akiwapimia eneo
na kuwa kila mmoja
alikuwa anapewa mita tatu za kujenga
kibanda japo wapo wengine
waliopewa zaidi .
Hata hivyo afisa
mtendaji wa kata ya Kitanzini aligoma kuzungumzia
suala hilo kwa madai
kuwa kwa sasa ni mtuhumiwa na
kulizungumzia na kwenda kinyume
na taratibu zake za kazi na atafika polisi kama
alivyotakiwa ili kutoa maelezo yake .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt Wiliam Mafwere alisema
kuwa wananchi hao wamevamia eneo
hilo na hakuna ruhusa ya uongozi
wa Halmashauri ya Manispaa kwa
wao kuvamia hifadhi hiyo ya
mlima Ipogolo .
Alisema wanazingatia
maagizo yote ya makamu wa Rais juu ya
uhifadhi wa mazingira na kuwa ni mara
kwa mara mkuu wa mkoa wa Iringa
anasisitiza juu ya ulinzi na usimamizi
wa hifadhi za mazingira.
Akiwa mkoani Iringa siku
tano zilizopita makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan
aliagiza viongozi wa mkoa wa Iringa kutunza mazingira na kuzuia wananchi kulima ama kujenga
katika hifadhi za milima kwa
ajili ya kuhifadhi ikolojia yam to Ruaha
mkuu ambayo imetoweka kutokana na
uharibifu wa mazingira unaofanywa na
wananchi huku mto
huo ukitegemewa na watu zaidi ya
milioni 8 pia Taifa kwa
ujumla kutokana na uzalishaji wa umeme
wa bwawa la Mtera na Kidato .
0 comments:
Post a Comment