Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka
17 Serengeti Boys jijini Dar es Salaam alipowaalika nyumbani kwake na
kupata nao chakula cha jioni kabla ya vijana hao
kuondoka Tanzania..kuelekea katika michuano ya mataifa ya Afrika ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon, Serengeti Boys
wanaondoka Aprili 5 kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya
michuano hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Dr Harrison
Mwakyembe akizungumza na kuwatakia vijana hao ambao wanakwenda
kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon.
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 Serengeti Boys ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania
katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17
itakayofanyika Gabon.
Picha zote na Philemon Solomon-www.mtazamonews.com
0 comments:
Post a Comment