METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 12, 2017

MADHARA YA UTAWAZAJI KWA WATOTO WETU MASHULENI

Na Creptone Madunda: Iringa

*Jambo la msingi lakuulizana au kujiuliza kwa mtu mzima yeyeto aliye na familia na asiye na familia kama anaweza kwenda chooni na kujisaidia akatoka bila kujitawaza na mwisho wa siku akajisikia vizuri au akajisikia kuwa huru?*

Bila shaka jibu ni hapana, mtu mweye utashi na akili zake timamu hatokuwa huru na hawezi kujisikia vizuri wala kuwa huru kama atashindwa kujitawaza baada ya kujisaidia, kwa masirahi mapana ya ustawi na maendeleo ya jamii zetu na taifa kwa ujumla ifike kipindi tuelezane UKWELI na kuweka udini, ukanda na itikadi za vyama pembeni na kueleza uhalisia wa mazingira hatarishi ya watoto wetu mashuleni .

Ni vyema tukatambua  kuwa tafiti zinasema zaidi ya asilimia themanini (80%) ya shule za sekondari na msingi zina vyoo visivyo na maji kwani upatikanaji wake ni wa shida hata zile zilizo na maji karibu zina miundo mbinu mibovu au hazina kabisa miundo mbinu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujitawaza baada ya kujisaidia.

SASA JIULIZE WEWE BABA, MAMA NA WEWE KIJANA HAWA WATOTO WETU WANAISHI NA KUSOMA KATIKA MAZINGIRA GANI ?

🔺Jiulizeni wasichana wa shule waliopo kwenye siku zao *"period"* wanapata shida kiasi gani, wewe ulipata shida kiasi gani ulipokuwa shule , watashindwaje kuaibika kutokana na hali hii,  je ungependa wanao, nduguzo na watanzania wenzako waendelee kuteseka kama ulivyoteseka ?

🔺Watashindwaje kupata magonjwa kama Urinary Track Infection (U T I), homa ya matumbo na magonjwa mengineyo yanayoweza kusababishwa na mazingira haya mabovu ya miundo mbinu ya vyoo ?

🔺Watashindwaje kutoroka na kwenda makwao kujisaidia au kwenda porini kujisitili na majani au nyasi ?

🔺Watashindwaje kushinda shule kutokana mazingira haya mabovu ya miundo mbinu ya vyoo kwa kusingizia kuumwa kipindi wanapokuwa kwenye siku zao *“period”*?

🔺Watashindwaje kujitawazia kwenye kuta, pembe za milango ya vyoo au kwa kutumia mawe au karatasi au njia nyingine zinazoweza kuwa sio salama kwa afya zao ?

🔺Watashindwaje kunuka darasani na kusabisha harufu mbaya darasani na kupelekea mazingira yasiyo rafiki kwa kujifunzia na kujisomea?

🔺Watoto watashindwaje kuathirika kisaikolojia na kuwafanya muda wote wawaze kuhusu hali ya harufu mbaya waliyo nayo inayoyoweza kuwa imesababishwa na wao kuwa kwenye siku zao au kushindwa kujitawaza baada ya kujisaidia?

*SWALI: Kwa mazingira hayo ni nani wakulaumiwa ?*

JIBU: Ni mimi, wewe na yule tulio amua kubaki kimya bila kuzungumza na kupaza sauti zetu kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira rafiki.

*NINI CHA KUFANYA?*

Wahoji viongozi wako wa kitaifa, mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa kuhusu changamoto hii uweze kujua mikakati iliyopo katika kulitatua tatizo hili.

Washirikishe wadau mbalimbali wa maendeleo jamii pamoja na wananchi wa sehemu unayoishi au sehemu uliyopo muweze kuangalia ni kwa namna gani suala hili linaweza kutatuliwa na kuwatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kusoma na kujifunzia.

*SOTE KWA PAMOJA TUWEKE ITIKADI ZETU PEMBENI TUZUNGUMZE UKWELI KATIKA MAZINGIRA YETU KUHUSU TATIZO HILI LA MIUNDOMBINU MIBOVU YA VYOO MASHULENI KWA MASIRAHI MAPANA YA WATOTO WETU, JAMII ZETU NA TAIFA KWA UJUMLA*.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com