Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliemshika bega) akitoa maelekezo kwa mkandarasi mradiMhandisi Emanuel Norbet wa miundombinu ya Umwagiliaji Wilaya ya Kiliosa kukabidhi mradi ifikiapo 30 Aprili 2020.Mkataba wa kazi umemalizika tarehe 21Aprili mwaka huu ambapo kazi imefikia asilimia 84.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof Riziki Shemdoe (aliyevaa kofia) alikagua mtambo wa kukoboa mpunga wa katika mradi wa ghala la kijiji cha Mvumi wilaya ya Kiliosa.Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya.
Ghala la kuhifadhia mpunga kijiji cha Mvumi wilaya ya Kilosa lenye uwezo wa kuhifadhi tani 1300 kwa mwaka likiwa limekamilika kwa asilimia 99 kwa gharama ya shilingi milioni 735 kati ya milioni 971 chini ya mradi wa ERPP.
Makatibu Wakuu wa Wizara nne leo wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji mkoani Morogoro na kuridhishwa na kukamilika kwa ghala la kuhifadhia mpunga kijiji cha Mvumi Wilaya ya Kilosa.
Ziara hii imewakutanisha Makatibu wakuu wa Wizara za Kilimo Gerald Kusaya,Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe,Naibu Katibu Mkuu OR -TAMISEMI Bw.Gerlad Mweli na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira Balozi Joseph Sokoine
Akizungumza kwenye ukaguzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya alisema ghala la kijiji cha Mvumi limekamilika na muda si mrefu litakabidhiwa kwa wakulima ili litumike .
" Wananchi wajipange kuanza kutumia ghala hili kwani kazi nzuri imefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kutoa fedha nyingi kujenga mradi huu ili usaidie kuongeza tija na thamani ya zao la mpunga kwa wakulima" alisema Bwa.Kusaya
Mradi wa ujenzi ghala la kijiji cha Mvumi chini ya mradi wa Kuongeza Uwezo wa Uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) umegharimu hadi sasa Shilingi milioni 735 kati ya 971 milioni utakapokamilika ambapo umefikia asilimia 99.3
Ghala Hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 1300 za mpunga kwa mwaka na litakuwa na kiwanda cha kukoboa mpunga chenye uwezo wa kukoboa kilo 1,200 kwa siku.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Gerlad Mweli amewataka wanakijiji cha Mvumi kujitolea kukamilisha ujenzi wa uzio wa ghala hilo ili kuimarisha ulinzi.eshauri utaratibu uwekwe kwa kila mkulima atakayetunza mazao yake ghalani kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Naye mkulima James Nkalalwe wa kijiji cha Mvumi ameishukuru Serikali kwa kukamilisha mradi huu kwani wanatarajia tija na uchumi wa wakulima uongezeke.
0 comments:
Post a Comment