Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Dkt Allan Kijazi akichangia mada kuhusu uhifadhi wa mto Ruaha mkuu
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akichangia mada juu ya uhifadhi wa mto Ruaha mkuu
washiriki wa mkutano huo wakitoa maoni yao
Mbunge wa Mary Mwanjelwa akichangia katika mkutano huo
Waziri wea Mazingira na muungano January Makamba akipokea maelekezo toka kwa makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akichangia jinsi ya kulinda mto Ruaha mkuu
Waziri wa Maliasili na utalii Dkt
Jumanne Maghembe akifafanua jinsi ya kuungana kulinda maji kwa faida
ya wananchi na wananya
Mbunge wa Makete Dkt Norman Sigalla
Na MatukiodaimaBlog
Akizungumza leo wakati wa mkutano wa kwanza wa kuhifadhi Ikolojia ya mto Ruaha alisema kuwa uwepo wa kikosi kazi hicho ni kuacha maneno na kuonyesha utendaji.
Alisema lengo la kuunda kikosi kazi hicho bila kwa sasa kushirikisha sekta binafsi ni kutaka kufagia nyumba yetu na kuona kasoro zilizojitokeza na baada ya hapo watashirikisha sekta binafsi.
Kwani alisema ushirikishwaji wa sekta zote ni muhimu kwa ajili yakunusuru mto Ruaha mkuu.
Huku akitaka wanahabari kushirikiana na kikosi kazi kuandaa vipindi vya elimu ya uhifadhi wa mto Ruaha mkuu na kuvirusha kwa wananchi.
Hata hivyo alisema kuwa kuwepo kwa kikosi kazi hicho hausimamishi sheria zilizopo katika uhifadhi wa mazingira na kutaka wizara zote kuungana kusimamia sheria za usimamizi bora wa maji.
Alisema kutokana na mgongano uliopo wa kila wizara kutetea eneo lake serikali imepoteza pesa nyingi sana katika uhifadhi na hivyo kutaka kuanzia sasa wizara zote kuungana kunusuru mto Ruaha mkuu.
Aidha alisema anaunga mkono wazo la mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam la kutaka kuangalia pia mito midogo.
Hata hivyo alitaka watumishi wote wanaoshindwa kutimiza wajibu wao kama mabwana shamba, misitu na wengine kufanya kazi kulingana na pesa wanazolipwa na kuwa serikali itaweka usimamizi sahihi kuona kila mmoja analipwa kulingana na kazi.
“Ni imani yangu kuwa kikosi kazi hiki cha kunusuru mto Ruaha kitafanya kazi yake vizuri “
Alisema kuwa Papa Francis alipata kusema kuwa Mungu ukimkosea atakusamehe ukitubu ila mazingira ukiyakosea hayatakusamehe.
0 comments:
Post a Comment