METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 10, 2017

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO YATEMBELEA NA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI MPIJI MAGOE



Na Nasri Bakari, Dar es Salaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia wataalamu kutoka Idara za kilimo, chakula na ushirika pamoja na mifugo na uvuvi wa Manispaa hiyo wamewatembelea na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima wa mpunga na wafugaji wa samaki Manispaa hiyo.

Tukio hilo limefanyika leo katika eneo la Mpiji Magoe, Kata ya Mbezi.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Afisa kilimo msaidizi wa Manispaa hiyo Ndg. Msafiri Charles Barnabas alisema wakulima inabidi wafate kanuni na kilimo bora na chenye tija hasa wakati huu wa palizi( kuondoa magugu).

"Wakulima inabidi mlime kilimo bora na chenye tija kwa kufuata kanuni zote za kitaalamu na pia muwe makini wakati wa kuchagua mbegu hizo" alisema Barnabas.

Akizungumza baada ya kupata elimu hiyo mkulima wa mpunga Ndg. Omari Kinemene Mangosonga alimshukuru sana Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo pamoja na wataalam hao kwa kuwajali wakulima wakubwa na wadogo.

Pia aliiomba Manispaa ya Ubungo kuwawekea mabomba (drip irrigation) sambamba na kutoa elimu juu ya matumizi ya mabomba hayo ili kuacha kutegemea mvua za msimu.

Wakati huo huo Afisa uvuvi wa Manispaa hiyo Bi. Maria Pentzel alisema mfugaji inabidi afate kanuni bora za ufugaji wa samaki kwa ku zingatia mbegu na chakura bora cha samaki.

Mwisho kabisa wataalamu hao waliwashauri wakulima wajihusishe na shughuli za kilimo mjini kwani kitawasaidia kujikwamua na maisha magumu kwa kuwaongezea kipato pia wafugaji wa samaki kabla ya kuanza ufugaji watafute ushauri wa kitaalamu ili kuepuka changamoto zitakazowakuta pindi watakapoanza ufugaji.

Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com