Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya kuanzia kushoto Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Raila Odinga na Moses Wetangula
Vigogo wanne wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanakutana
Pwani ya nchi hiyo kujadiliana na kuamua ni nani kati yao
atakayepeperusha bendera ya muungano huo wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi
Agosti.
Hatua hii inakuja baada ya watalaam
waliokuwa wamepewa jukumu la kumtafuta mgombea wa upinzani kumaliza kazi
yao na kutoa mapendekezo yao kwa wanasiasa hao wanne kufanya maamuzi ya
mwisho.
Wanasiasa hao wanaotafuta tiketi ya muungano huo kupambana na rais Uhuru Kenyatta
anayetafuta muhula wa pili ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila
Odinga, aliyekuwa Makamu wa rais Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na
Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Moses Wetangula.
Vyombo vya Habari nchini Kenya
vinaripoti kuwa, duru kutoka katika kamati ya watalaam imependekeza kuwa
Raila Odinga awe mgombea urais huku Kalonzo Musyoka awe mgombea mwenza
wake kama ilivyokuwa mwaka 2013.
Musalia Mudavadi inapendekezwa kuwa awe
Waziri Mkuu huku Moses Wentangula akipewa Uspika au kiongozi wa walio
wengi bungeni ikiwa muungano huo utashinda uchaguzi huo.
Wanasiasa hao wanakutana kwa muda wa
siku tatu zijazo, huku ikitarajiwa kuwa mgombea wa upinzani akitazamiwa
kutangazwa wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment