METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 1, 2017

DC STAKI ASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ameshiriki Zoezi la upandaji miti lililofanyika Katika kingo ya mto Pangani, Kijiji cha Mferejini, Kata ya Ruvu.

Katika zoezi hilo lililofanyika kiwilaya jumla ya miti 34000 imepandwa ambayo ni  wastani wa miti 1000 katika kila kata.

Alizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Dc Staki alisema kuwa zoezi hilo limewahusisha wadau mbalimbali pamoja na Pangani River Basin.

Mhe Staki ameitaka Pangani River Basin  kuweka mkakati madhubuti wa kuulinda mto huo na kuuimarisha ili kuakisi upatikanaji maji kwa wingi zaidi kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya amewasihi kuishirikisha ofisi yake Na kushirikisha  wafaidika wote waliopitiwa na mto huo kama watekelezaji wa mpango huo mahususi.

Staki amewataka Pangani River Basin kuweka Alama maalumu (Bicon)  kuonyesha Mita 60 zinapoishia ili wananchi kutambua alama hizo.

Pia amewaagiza Viongozi wa vijiji, vitongoji na kata kusimamia sheria kwa kuwachukulia hatua wananchi wote wanaovunja sheria.

"Kila mti unaopandwa ni lazima ukue, Sitaki kusikia mti umekufa kwa kukosa maji, mchwa au mifugo. Sisi tumepewa akili na utashi, Tumepewa mamlaka juu ya viumbe vyote, Hakuna cha kutushinda, Tutafute maarifa ili miti hiyo ikue". Alisisitiza Mhe Senyamule.

Wilaya ya Same inapitiwa na kilomita Zaidi ya 100 ya mto Pangani kati ya kilomita 500 za mto huo ambapo Wilaya inapanga kuutumia mto huo kwa shughuli za umwagiliaji katika kata ya Ruvu ili kukuza uchumi wa wananchi wake.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com