METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 19, 2017

CLINIC TEMBEZI YAFUNGULIWA KONGWA

Na Peter Daffi

Wilaya ya Kongwa imefungua rasmi zoezi la clinic tembezi, ambapo madaktari bingwa wa magonjwa mbali mbali watatoa huduma kwa wananchi wa Kongwa kwa muda wa siku 7.

Mkuu wa wilaya ya kongwa Mh Deo ndejembi amewahimiza wananchi wa Kongwa kujitokeza kwa wingi kupata tiba.

Ndejembi amesema kuwa Pana madaktari Bingwa Tisa (9) wakutibu magonjwa mbali mbali ya Kina Mama, Watoto, Wazee, Wataalamu wa Masikio, Pua Macho, Ngozi, na magonjwa mengine.

DC Ndejembi anasema Tunakaribishwa kwa Wingi kujitokeza kutibiwa kwani Huduma hii inapunguza usumbufu wakutembea na kupunguza garama kwenda Hospitali.

Uzinduzi ulifanywa na Naibu waziri wa Afya Dkt Kigwangalla

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com