METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

ASASI YA AWAMATA YAMKABIDHI CHETI CHA PONGEZI MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha cheti alichokabidhiwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi (Katikati) akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Hindu Lugome ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya ustawi wa Jamii, Watoto na Wazee Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) (Kulia), Mwingine ni Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Bi Millensasha Mneo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi (Katikati) akizungumza na viongozi wa AWAMATA mara baada ya kukabidhiwa cheti cha Pongezi ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam, Kulia ni Hindu Lugome ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya ustawi wa Jamii, Watoto na Wazee Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) (Kulia), Mwingine ni Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Mkoa wa Dar es salaam Bi Millensasha Mneo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo (Aprili 18, 2017) amekabidhiwa cheti cha Pongezi kutoka kwa viongozi wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika Manispaa ya Ubungo na Taifa kwa ujumla katika utendaji wa kazi za jamii.

Cheti cha Pongezi kimetolewa na Mwenyekiti-Taifa wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Chief Mrindoo Babu Mwidadi kwa MD Kayombo ambapo kwa niaba yake kimekabidhiwa  na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya ustawi wa Jamii, Watoto na Wazee Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Bi Hindu Lugome sambamba na Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Mkoa wa Dar es salaam Bi Millensasha Mneo.

Akizungumza mara baada ya dhifa ya makabidhiano ya cheti hicho yaliyofanyika Katika Ofisi ya Manispaa ya Ubungo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg John Lipesi Kayombo ameishukuru Asasi ya AWAMATA kwa kutambua mchango wake katika kuwatumikia wananchi wa Manispaa ya Ubungo ambapo amebainisha kuwa hilo ni jukumu la kila kiongozi wa serikali nchini katika kuwatumikia wananchi ili kuboresha maisha yao na kupelekea Taifa kufikia katika uchumi wa kipato cha kati.

Alisema kuwa miongoni mwa ndoto za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni pamoja na kuwainua watanzania wanyone kufurahia maisha katika nchi yao ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukemea wizi na ubadhilifu uliokuwa unafanywa na viongozi wachache katika serikali hivyo akiwa mratibu wa shughuli zote za Manispaa atahakikisha anasimamia kauli mbiu ya serikali ya HapaKaziTu kwa manufaa ya watazania wote.

MD Kayombo amesema kuwa serikali kwa kipindi kirefu imekuwa ikinyooshewa kidole na wananchi wake kutokana na kuwafumbia macho wabadhilifu wachache wa mali za Umma lakini kwa sasa wamefikia ukomo kutokana na weledi wa utendaji wa Rais sambamba na watumishi wengi wote ambao wanamsaidia Rais kukamilisha majukumu yake katika maeneo yao ya kazi.

Naye Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Mkoa wa Dar es salaam Bi Millensasha Mneo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti-Taifa wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Chief Mrindoo Babu Mwidadi amesema kuwa Cheti hicho kimetolewa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kutokana na umakini wake katika utendaji kwani anaigusa jamii moja kwa moja na anafanya kazi za umakini mkubwa huku kazi hiyo ikioneka wazi.

"Sisi hatutoi cheti kwa kiongozi ilimradi ni kiongozi tu bali tunatoa cheti kwa kiongozi muwajibikaji na mweledi katika utendaji" Alisema Bi Mneo

AWAMATA ni Asasi isiyokuwa na kiserikali iliyosajiliwa kwa mujibu na taratibu za kisheria nchini, inajishughulisha na mambo ya kijamii hususani katika kusaidia makundi mbalimbali ya watoto yatima, wajane, walemavu na wasiojiweza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com