METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

MADEREVA WA DALADALA WASHUKURU JIJI LA ARUSHA KUPITIA MKURUGENZI KWA KUWAKARABATIA BARABARA YA KROKONI


Na Mwandishi Wetu,Arusha

Waendesha daladala za kwenda Njiro kwa msola,Moshono,Kijenge Uswahili,na Ungalimitedi pamoja na makondakta wamempongeza Mkurugenzi wa Jiji La Arusha Bwana Athumani Juma Kihamia kwa kuwasaidia kukarabati barabara ya Krokoni ambayo ilikuwa tatizo ikiwemo mashimo ambayo yalikuwa yanawafanya kila wakati kutengeneza magari yao.

Malalamiko ya barabara hiyo ambayo yaliwasilishwa kupitia Triple A Radio kwenye kipind cha Jambo Tanzania kuhusu barabara hiyo wamesema kuwa licha ya kwamba haijakarabatiwa kwa ubora ule unaotakiwa lakini imepunguza adha ile waliyokuwa wanapata.

"""Eee bwana sisi kama madreva Mungu amuongezee miaka mingi huyu Mkurugenz Kihamia sisi hatumjui lakini alipotusikia tunalalamika kupitia Triple A ametusaidia huyu ndiyo kiongozi anaeheshimu wananchi wake tunamuomba aendelee hivyo hivyo "" walisema madreva

Wameongeza kuwa kila Siku walikuwa wanatengeneza magari yaliyokuwa yanaharibika kwasababu ya ubovu wa barabara ya Krokoni hivyo kipato walichokuwa wanapata walikuwa wanatengenezea magari.

Wameleza kuwa kupitia ubovu wa barabara hiyo mpaka madreva wengine wamepoteza kazi kwasababu wanapowaeleza kuwa Fedha wanazopata wakati mwingine zinatumika kutengeneza barabara hawaelewi hivyo kuachishwa kazi.

""Yani kila Siku bush za gari zilikuwa zinakufa kwahyo ukienda kumwambia tajiri umenunua kifaa ukatengeneza gari haelewi anakuambia lete gari mana kazi imekushinda unaingiza hasara sasa yani tunashukuru tutaendelea kulinda vibarua""

Kwa upande wa Mkurugenzi Bwana Kihamia amewataka wananchi waendelee kushirikana ili kuboresha baadhi ya vitu ambavyo vina changamoto kuliko kunyamaza na kuendelea kulalamika na kuilaumu serikali na kuumia kwa kuwa yupo kwa ajili ya wananchi.

"" Yani Mimi kama Mtendaji mkuu wa Halmashauri ya Jiji nawaomba wananchi wetu wakiwa na tatizo wasilalamike kwasababu wakilalamika hakuna msaada lakini kusaidika kwao ni kwa kusema ili tuwasaidi kwasababu tuko kwa ajili yao"" alisema Kihamia
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com