METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 29, 2016

Mambo matatu muhimu ya kuyajua kuhusu chungwa na faida zake

Leo napenda ufahamu kuwa endapo utapata nafasi ya kula angalau chungwa moja tu kila siku basi tambua wazi kuwa kuna hizi faida hapa chini utakuwa unazzipata kila unapotumia tunda hilo.

Kwanza utauhakikishia mwili wako usalama mkubwa zaidi wa kiafya kutokana na tunda hilo kuwa na kiwango cha kutosha cha vitamin C ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kumfanya mhusiaka kutosongwa na magonjwa ya mara kwa mara kirahisi.Lakini pia ulaji wa chungwa mara kwa mara utaupatia mwili wako madini ya potassium, calcium, folate, pamoja na vitamin B ambavyo vyote kwa pamoja ni muhimu ndani ya miili yetu wanadamu.

Pamoja na hayo, chungwa pia lina nyuzinyuzi 'fiber' ambazo huhitajika sana katika kufanya zoezi la umeng'enyaji chakula ndani ya tumbo na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa choo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com